Leo jiulize swali hili la muhimu kwenye maisha yako. Tukitaka kupima thamani yako kwa mawe ya ardhini utafanana na mchanga au almasi?
Kama tunavyojua almasi inapatikana kwenye miamba migumu chini kabisa ya ardhi. Almasi ili uweze kuichimba kama hutumii mashine utahitaji wanaume wenye nguvu sana.
Mchanga utahitaji vijana kadhaa na makoleo kadhaa tu wakapakie.
Bei ya mchanga lori moja ni rahisi sana lakini yote ni mawe, yote yanatoka chini.
Kinachofanya almasi iwe ghali kiasi kwamba ukipata kipande kidogo unakuwa tajiri ni kwasababu ya upatikanaji wake.
Tunajifunza nini hapo kama wanadamu?  Kama wewe utakuwa na sifa za mchanga thamani yako itashuka. Thamani ikishuka hata matumizi yako yatakuwa ni ya kawaida.
Ukihitaji mchanga unaenda mtoni tu kuchota hata na ndoo. Ukihitaji almasi inaweza kukuchukua miaka kadhaa ukichimba hadi uifikie.
Kama wewe ni mwanamke usikubali kuwa aina ya mwanamke ambaye kila mwanaume akimhitaji anaweza kumpata kirahisi.
Kama unaweza kupatikana kwa ofa ya chipsi kuku na soda thamani yako ndio hiyo.
Hujawahi kusikia mtaani vijana wanasema ” binti fulani  ukimtaka wewe mnunulie chips kuku tu”
Yaani maanake wewe thamani ya mwili wako ni viazi na kuku.
Soma: Thamani ya Kitu
Mwanaume usikubali kuwa wa hovyo. Kila mwanamke anaweza kuwa wako,  kila mwanamke unamtongoza? Wewe thamani yako inafanana na vile unavyovichagua.
Mwanamke usipatikane kirahisi. Ukiona gari unaweweseka. Ukionyeshwa simu ya milioni unavua nguo. Embu watazame wanawake wenzako wenye majina makubwa wangevuliwa nguo kwa simu wasingesikika huku duniani.
Thamani yako ni kusudi la Mungu aloweka ndani yako.
Thamani yako ni Maono makubwa uliyonayo.
Thamani yako ni ndoto yako kubwa uliyonayo.
Usikubali kukaa kaa hovyo,  hata kama huna pesa. Usijirahisishe kwa kila mtu kwasababu tu una shida fulani. Unadhalilisha maono na kusudi lililopo ndani yako.
Mungu hajakosea kukuumba Mrembo. Angeweza kukuumba yeyote yule. Tumia uzuri ulionao kwa manufaa ya kusudi lako.
Mwanaume nguvu ulizonazo sio za kutumia kwa wanawake. Una nguvu kwa ajili ya kusudi la Mungu.
Tumia nguvu hizo kujitengenezea njia na baadae yako nzuri.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading