Kabla Hujafanya jambo lolote unashauriwa uangalie mwisho wako utakuaje. Hakikisha umeona mwishoni ni matokeo gani utapata. Kama ni mahusiano mapya embu tazama mwisho wake kabla hujaingia. Unataka kuanza biashara tazama mwisho wake. Lakini tukumbuke pia kama unafanya mambo yasiyofaa embu jaribu kuona mwisho wake. Embu jaribu kuona madhara ya tabia mbaya ulizonazo? Unafikiri utakuwa na Maisha ya aina gani baada ya miaka kadhaa?

Jiulize swali baada ya kuona mwisho wa mazuri unayofanya, Jiulize Itakuaje? Kama usipofanya hiyo biashara itakuaje? Hali uliyonayo sasa hivi itakuaje miaka mitatu ijayo? Itakuaje usipofanya mabadiliko ya tabia mbaya uliyonayo?
Itakuaje ndoa yako kama bado unaendelea na michepuko? Itakuaje afya yako kama bado hutaki kufanya mazoezi na unaendelea kula vyakula visivyo bora? Itakuaje kama utaendelea kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii kufuatilia habari za kusisimua huku muda wako ukipotea bure?
Itakuaje kama utaendelea na tabia yako ya kutumia pesa zote bila ya kuweka akiba? Itakuaje kama utaendelea kubakia na ufahamu huo huo ulio nao siku zote? Hutaki kusoma vitabu, unafikiri Maisha yako yatakuaje?
Itakuaje kama utaendelea na tabia ya ulevi uliyonayo? Sigara unazovuta ukiendelea kila siku miaka kadhaa ijayo utakuwa mtu wa namna gani? Unaendelea kung’ang’ania ajira hutaki kuweka mpango wa kujiajiri na kuongeza kipato chako embu jiulize itakuaje siku umefukuzwa hapo kazini?
Mara ya mwisho kwenda kusali kule unaposali ni lini? Jiulize itakuaje juu ya Imani yako? utakuwa mtu wa namna gani kama utaendelea na tabia hiyo? Jiweke kwenye nafasi ya watu ambao umeona Maisha yao yameharibika baada ya kumwacha Mungu. Je upo tayari kufika huko walipo?
Jiweke kwenye nafasi ya watu wanaowa magonjwa ya presha kwa ulaji mbovu. Je upo tayari kufika huko? Upo tayari kuja kuugua magonjwa ya zinaa kwasababu ya tabia zako za kutembea hovyo na kila anaekuja mbele yako?
Baada ya kujiuliza maswali haya muhimu ni vyema ukaamua sasa kubadilika. Kama ni tabia mbovu ulikuwa nayo embua anza kuiacha. Kama kuna sehemu ya kubadilisha badilisha haraka kabla hayo mabaya uliyoyaona hayajakufika.
#USIISHIE NJIANI

Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading