Watu wengi tumekuwa na tabia za kuanza vitu vipya mara kwa mara na kuishia njiani bila kuvikamilisha. Zipo sababu nyingi ambazo zimekuwa zinachangia kufanya watu waache vitu vile walivyoamua kuvifanya. Leo utapata kufahamu baadhi ya vitu ambavyo vimewazuia wengi sana.

Kutokujua Kwanini wameamua Kufanya.

Unaweza kujua jinsi ya kuuza duka lakini kama hujui kwanini unauza duka ni rahisi sana kukata tamaa. Kwanini yako ndio inatakiwa iwe msukumo wako wa kwanza kwenye kufanya maamuzi ya vitu unavyokutana navyo kila siku. Mfano umekutana na fursa mpya leo imekuhamasisha sana kabla hujaamua kufanya jiulize kwanini niifanye? Kwanini hii na sio nyingine zitakazokuja au zilizopita? Ukiweza kujua kwanini utapata nguvu kubwa ya kuendelea mbele na kufikia mafanikio.

Kukosa Maono.

Watu wengi hawana maono hivyo kujikuta wanafukuzana na kila kinachokuja mbele yao. Inaweza kuja hata biashara ya kitapeli kwasababu huna maono huwezi kujiuliza mara mbili kama kweli biashara hiyo itakuwezesha wewe ufike sehemu Fulani au itakuharibia maono yako. Kwasababu ya wengi kutokujua wanapokwenda wanachukuliwa na kila linalokuja mbele yao kwa kuhamasishwa na mafanikio ya wengine. Kama utaanza biashara au kitu chochote kwasababu umeona watu Fulani wamefanya wakafanikiwa ni rahisi sana kuishia njiani.

Hakikisha una maono yako makubwa sana. Fanya juhudi za kila namna ambazo ni sahihi kufikia maono yako. Usibebwe na kila linalokuja mbele yako hakikisha umejua linaweza kuleta matokeo chanya kwenye maono yako.

Soma: Fanya Mambo haya Ndoto Yako Ikatimie

Kutokujifunza.

Uvivu wa kusoma vitabu umekuwa chanzo cha wengi kuishia njiani. Mtu anakata tamaa kabla hajafikirisha akili yake juu ya suluhisho. Mtu anakata tamaa na kuacha kile alichokuwa anakifanya ukimuuliza amesoma vitabu vingapi juu ya kile anachokifanya  atakwambia hajasoma. Ukimuuliza alikua anajifunza kwa nani hana mtu anaejifunza kwake.

Ili usiishie njiani hakikisha una taarifa za kutosha juu ya kile unachokifanya. Hakikisha unasoma vitabu kila wakati. Hakikisha unaomba msaada kwa waliofanikiwa na wahamasishaji au waalimu kama mimi huku. Utaelekezwa au kuunganishwa na watu ambao wataweza kukusaidia.

Tukutane tena kesho kwenye sababu nyingine za watu kuishia njiani.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading