HATUA YA 174: Kwanini Watu Wengi wanaishia Njiani? (2)

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Yapo mambo mbalimbali tunaanza kila siku lakini mwisho wake hatufiki. Wengine wanaingie kwenye mahusiano kwa lengo la kuoana lakini wanaishia njiani. Wengine wanaingia kwenye biashara kwa lengo la kufikia hatua Fulani kubwa lakini hawafiki wanaishia njiani. Zipo sababu nyingi ambazo zinaweza kuchangia mambo haya kutokea. Lakini nimeendelea kukuonyesha baadhi ya mambo mengine ambayo yanakuwa sababu ya kutufanya tuishie njiani.

Kukosa Maandalizi.

Kama utaanza jambo bila ya kujiandaa vya kutosha ni rahisi sana kuishia njiani. Ninaposema kujiandaa simaanishi vitu vya nje ila namaanisha ndani yako mwenyewe. Kuanzia ndani yako uwe tayari kukutana na changamoto, uwe tayari kukutana na vikwazo na upambane navyo.

Kujiandaa kutoka ndani yako ukiwa unafahamu kabisa mwisho wa kile unachokianza. Hivyo unakuwa unapambana ukijua ni wapi unakwenda.

Kukosa Hamasa.

Kama utakosa hamasa ya kufanya kile unachokifanya ni rahisi sana kuacha. Kama utakosa hamasa kwenye mahusiano yako ni rahisi sana kuachana. Hamasa inatusaidia sana hasa pale tunapopitia kwenye nyakati ngumu ambazo hazina majibu. Hamasa ndio inaweza kuwa sababu ya kutupa ujasiri wa kuyaendea yale tunayoyaona magumu.

Usikubali kupoteza hamasa yako. fanya vitu vile ambavyo vinaamsha hamasa yako pale unapojiona unaipoteza.

Kutokujitoa kikamilifu kwa ajili ya kile unachokifanya au kwa ajili ya vitu vingine kama mahusiano ni rahisi sana kuishia njiani. Lazima uamue kabisa kwamba safari uliyokubali kuiendea sio ya kawaida na umekubali basi lipa gharama. Mtu yeyote anaekata tamaa mara nyingi akiwa hana sababu ya msingi utagundua hakujitoa kikamilifu kwa ajili ya jambo lenyewe.

USIFANYE MAMBO NUSU NUSU UTAPATA MATOKEO NUSU NUSU. KAMA UMEAMUA KUFANYA FANYA, KAMA UMEAMUA KUACHA ACHA.

Kuendelea kufanya jambo ambalo unajua hakika hutafika nalo mwisho ni kupoteza muda.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading