Kuna watu wawili ambao siku zote ndio wanakuwa sababu ya kukurudisha nyuma kwenye safari yako ya mafanikio watu hawa unatakiwa uwe nao makini ili usiwasikilize. Wanasema ukimfahamu adui yako ni nusu ya kumwangamiza. Watu hawa wawili ndio unatakiwa uwaelewe vizuri sana.
“There are two types of people who will tell you that you cannot make a difference in this world: those who are afraid to try and those who are afraid you will succeed.”
– Ray Goforth
– Ray Goforth
Kuna aina mbili ya watu ambao watakwambi huwezi kufanya mabadiliko kwenye dunia hii. Ni wale wanaoogopa kujaribu na wale wanaoogopa utafanikiwa.
Wanaoogopa kujaribu ndio wa kwanza kabisa wala kutokuwasikiliza kile wanachokisema kwasababu wanakuogopesha kwenye kitu wasichokijua wenyewe. Wanakueleza maneno ya kusikia.
Watu ambao hawajawahi kujaribu kwenye hii dunia wana hadithi nyingi kwanini wao hawajaweza. Wanaweza kukueleza sababu elfu moja kwanini wao hawajaweza lakini sababu hizo haziwasaidii chochote. Haziwatoi pale walipo.
Binadamu ambao wanakwambia hutaweza kwasababu tu wanaona wivu na kuogopa utafanikiwa unatakiwa uwapuuze kabisa. Hawa unatakiwa ukae nao mbali sana kwasababu wanaweza kufanya chochote ili tu usisonge mbele. Hutakiwi kabisa kuwaeleza mambo unayofanya acha tu wasikie kwa wengine.
Hawa ni aina ya watu ambao wanatamani wao peke yao ndio waonekane wamefanya jambo kwenye jamii. Wana roho za ubinafsi. Kama ulishasikia mafisadi basi hawa wana roho za kifisadi.
Utawezaje kuwagundua watu hawa?
Yeyote anaekuja kwako na kukueleza kwamba hutaweza au achana na hicho kitu unachokifanya muulize au chunguza kwanza yeye anafanya nini. Ukishajua utapata jibu sahihi. Kama mtu huyo hajawahi kufanya basi ujue amekuja kukuambukiza hofu zake tu.
USIKUBALI HOFU ZA WENGINE ZIKAE NDANI YAKO, HADI UNAFIKIA KUFANYA MAAMUZI NI UJASIRI TOSHA WA KUKUWEZESHA WEWE KUSONGA MBELE. KAA NA WASHINDI WENZAKO.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com