“Tangu Kipindi Kile Unasema utafanya mambo yakikaa sawa Yalishakaa sawa?”
Nitaanza kuweka akiba mambo yakikaa sawa.
Nitaanza hiyo biashara mambo yakikaa sawa.
Nitajiunga mambo yakikaa sawa.
Mambo yakikaa sawa imekuwa ni sababu ambayo wengi wanaitumia ili kuepuka kufanya mambo mbalimbali yanayowahitaji. Ukweli hakuna siku mambo yanakaa sawa na ukiona mambo yamekaa sawa wala hutakumbuka tena kama ulikuwa unataka kuanza biashara kwasababu mambo yameshakaa sawa.
Ukweli ndio huo kama unafikiri huna pesa sasa hivi ndio maana huweki akiba basi anza kuitafuta pesa ili uweke akiba ukisema unasubiria mambo yakae sawa hutakaa ujue ni lini yamekaa sawa.
Soma: Tabia Ya Kuahirisha Mambo
Kama hujajitoa kwenye jambo kweli kweli utaishia kusema mambo yakikaa sawa nitafanya badala ya kwenda kuyaweka sawa hayo mambo. Mambo hayakai sawa yenyewe lazima utoke ufanye kitu. Badala ya kusema mambo yakikaa sawa embu fikiria mbele Zaidi unayafanyaje sasa hayo mambo yakae sawa?
Usikubali kuishia kwenye sababu nenda mbele Zaidi utatatuaje hiyo sababu uliyonayo sasa hivi. Kama huna mtaji basi usikae unasubiri mtaji uje tafuta kitu cha kufanya.
Jitazame ujuzi ulionao, vitu ulivyonavyo (unavyomiliki), mazingiria uliyopo, angalia ni namna gani unaweza kutumia ili utatua changamoto zinazokufanya useme mambo yakikaa sawa.
MAMBO HAYAWI SAWA YENYEWE, HAKUNA MTU MWINGINE ANAWAZA JUU YA MAISHA YAKO KULIKO WEWE MWENYEWE. ANZA KUYAWEKA SAWA MAMBO YAKO.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading