Wakati mwingine inakubidi ujitoe sadaka tu kama mambo hayaendi.  Umeona hakuna njia inayofaa katika zile zote ulizokuwa unazitarajia.

Kuna nyakati sasa inakubidi ufanye jambo la tofauti kabisa. Kiasi ambacho kila utakaemueleza anaweza asikuelewe.

Kama maamuzi mengi unayotaka kufanya kila mtu anakutia moyo kwa kukwambia nenda kafanye jua hayo sio maamuzi magumu.

Kuna nyakati hata wale uliozoea kuwaomba ushauri wanasema hapana hilo unalotaka kufanya halifai. Huko unakotaka kwenda unapotea kabisa.

Hapo sasa ndio unatakiwa usimamie kile ulichokiona na unachokipigania.

Kuna maamuzi ukifanya hata yule wa karibu yako kabisa anakosa matumaini. Anaanza kuona maisha yatasimama lakini kwasababu hakuna namna nyingine yaani ni kubaki ulivyo na umaskini wako au kufanya jambo la kuhatarisha maisha yako.

Unajua mafanikio ni gharama. Kiwango cha mafanikio uliyonayo sasa hivi ni kiwango cha gharama uliyolipa.

Kwenye kulipa gharama wakati mwingine unaweza kupata hasara.

Jitoe sadaka sasa kama umechoka na hali unayoendelea nayo.

Fanya kitu cha tofauti kabisa ambacho watu wachache sana ndio watakutia moyo,  au hata wote watakupinga.

Bila ya kujitoa sadaka wakati mwingine huwezi kupata ulichokuwa unakitaka.

Chukulia mfano wa maisha ni kama safari ya porini. Katika pitapita zako umekutana na chui mkubwa anakukimbiza. Katika kukimbia ukakutana na mto mkubwa mbele yako. Nyuma anakuja chui kwa kasi.  Ili kuyaokoa maisha yako namna iliyobaki ni kutumbukia kwenye maji tu.

Bahati mbaya sana wewe hujui kuogelea kabisa. Sasa hapo unachagua moja utumbukie kwenye maji ujifunze kuogelea tu ukiwa ndani ya mto,  au uliwe na chui.

Maisha wakati mwingine yanaweza kuwa kama safari ya porini. Ugumu wa maisha na umaskini ndio chui mwenyewe anaetukimbiza.  Mto ndio suluhisho lililobaki yaaani uingie kwenye biashara au ubaki hivyo ulivyo uliwe na umaskini. Ufanye kitu cha tofauti au uendelee na mazoea umaskini ukume?

Chagua moja kama hali uliyonayo imekuchosha. Usipofanya jambo la tofauti hali itazidi kuwa mbaya zaidi.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading