“Tangu nilipoacha kulalamika, nilipoacha kulaumu wengine kwa changamoto ninazopitia, nilipoacha kusema fulani alipaswa kunisaidia, alipaswa kunitafutia kazi, alipaswa kunisomesha, hapo ndipo nilianza kuona mabadiliko kwenye maisha yangu.” Jacob Mushi.

Kabla hujaanza kuona kwamba unastahili kusaidiwa kitu Fulani wewe binafsi una nafasi gani ya kumwezesha mtu? Inawezekana kwa nguvu zako, kwa maarifa uliyonayo au chochote kilichopo ndani yuako.

Usikubali kuwa mtu wa kuonewa huruma hasa kwenye mambo ambayo ulipaswa kuyatatua mwenyewe. Kuna nyakati nilikua napitia ngumu sana. Marafiki zangu wananiambia wewe kaka yako si akutafutie kazi? Kwa bahati mbaya sana sikuwa na maarifa ya kutosha nikabaki naona ni kweli nastahili kutafutiwa kazi na kaka. Kumbe hakuna kitu kama hicho nikienda kwa kaka ndio nagundua kwamba hata kazi zina changamoto zake kubwa sana.

Nilipoanza kusoma vitabu nikaanza kuelewa kwanini hasa sitakiwi kulalamikia wengine. Kama una mikono na miguu yako miwili jitume kwa kutumia ujuzi ulionao, kipaji chako na hata nguvu zako. Watu wataona kazi yako ndipo njia zitafunguka. Ukikaa sehemu moja unasema baba anajua sina kazi, mjomba anaelewa nimemaliza shule nikafeli, hakuna kitakachobadilika kwenye Maisha yako.

Wajibika kwa ajili ya Maisha yako mwenyewe. Kama hakuna chochote unachofanya embu fanya namna sasa hivi uanze kutoka hapo ulipoganda. Hakuna mafanikio yanayokuja hivi hivi. Usiwaone watu wamepiga hatua ukafikiri wameanzia hewani.

Lazima ukubali kuanza kitu peke yako ndipo watu waone juhudi zako. Kabla hujaomba msaada wowote hakikisha umeshaweka juhudi za kutosha hadi unaona kama imeshindikana hivi ndipo uombe msaada.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading