HATUA YA 18: Usiishie Njiani.

By | January 1, 2017

Heri Ya Mwaka Mpya.
Nina neno moja tu kwako mwaka huu wa 2017. #USIISHIE NJIANI.
Yapo mengi sana Ulianza mwaka jana ukaweka malengo makubwa lakini ukaishia njiani. Mwaka huu sio wa kuishia njiani. Mwaka huu ni wa kumaliza ulichokianza. Mwaka huu ni wa kufikia mafanikio makubwa.
Mwaka 2017 ni wa kwako wa Kupiga hatua.
Mwaka 2017 Nataka niandike hadithi ya Mafanikio yako ndani ya mtandao huu. Hivyo nakusihi sana Usiishie Njiani.
Mwaka 2017 tutakuwa pamoja kila siku hapa tukitiana moyo. Ninakuahidi sitakuacha njiani tutaenda pamoja naomba na wewe usiniache  njiani.
Je upo tayari tuanze mwaka pamoja kwa kushirikishana haya mambo mazuri?  Upo tayari kufanyia kazi unayojifunza hapa? 
Kama upo tayari basi na mimi nipo tayari kwenda pamoja na wewe.
Nimekuahidi kitu kimoja hadithi yako ya Mafanikio itaandikwa kwenye mtandao huu
Ili tusiishie njiani Naomba unipe uhakika wako kwa kunitumia email au ujumbe kwa njia ya wasap kwamba tutakuwa pamoja mwaka 2017.
Ninataka nifanye kazi pamoja na wewe. Ninatamani upige hatua. Ninatamani Uinuke na Kisha Uangaze.
Karibu sana Rafiki Yangu. Usiache kuniandikia kama tutakuwa pamoja.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/ +255 755 192 418

jacobmushi.com.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *