Unachotakiwa kukumbuka ni kwamba unapokuwa na mteja wako hata saa moja usionyeshe uso wa hasira hata kama atakuwa amefanya mambo ambayo siyo mazuri. Hata kama mteja amekukasirisha kwa kutokuelewa kwake usimwonyeshe kuchukia ama kukasirika.
Tabasamu ndio silaha ya pekee ya kumvutia mteja aje kwako mara kwa mara. Kumbuka mteja wako ameteseka sana kuitafuta pesa yake halafu akaamua aje kwenye biashara yako na sio mahali pengine akupe pesa umpe huduma au bidhaa yako. Kama utakosea na kumwonyesha hasira au kutokumjali lazima ataondoka maana ataona kama anapoteza pesa yake.
Haijalishi biashara yako ni ngumu kiasi gani kipindi hicho usikubali iwe sababu yaw ewe kuwanunia wateja wako. Tabasamu ndio kila kitu kwenye biashara yako. linaweza kumfanya mteja ambaye alikua hajapanga kununua kitu akanunua kwasababu ya tabasamu lako.
Tabasamu ni uponyaji wa nafsi zilizopo kwenye mawazo, majonzi, maumivu, uchovu, na mengine mengi. Ukiweza kulitumia vyema tabasamu basi kila mteja atakuwa wako. Wafanye wateja wasikie furaha wanapokuwa kwenye biashara yako.
Soma: Kitu cha Muhimu Kwenye Biashara Yako Ni Hiki
Wafanye wateja wasahau kidogo hali mbalimbali wanazopitia kwenye Maisha yao kwa muda ule mfupi wanaokuwa kwenye biashara yako. Yote haya unaweza kuyafanya kwa kuonyesha tabasamu tu.
Ili uweze kuwa na tabasamu kila wakati kwenye biashara yako unahitaji sana kuipenda biashara yako. Unahitaji kupenda sana hicho unachokifanya. Itakuwia vigumu sana kuvumilia wateja wanaokera kama hupendi unachokifanya.
Hata kama umeajiri mtu mfundishe namna ya kukaa kwenye biashara yako. Mfanye aipende kazi yake akiipenda kazi yake ataweza kuvumilia yote atakayokumbana nayo kwenye kuwahudumia wateja.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading