HATUA YA 183: Chanzo ni Nini?

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Hakuna kitu kinatokea chenyewe bila ya kuwepo kisababishi. Kama sasa hivi huna pesa kuna chanzo cha wewe kukosa pesa. Ukitumia muda mwingi kulalamika kwamba huna pesa utakuwa unapoteza muda. Badala yake tumia muda huo kujua nini chanzo cha wewe kukosa pesa.

Umepitia changamoto yeyote kwenye Maisha yako badala ya kuumia sana, na pia kabla hujaanza kuomba ushauri kaa chini jiulize chanzo cha chake. Unapodahamu chanzo unakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutatua.

Kuna matatizo mengine tunapitia halafu tunabakia kuwalaumu wengine lakini tukikaa chini na tukatafakari unakuja kugundua chanzo cha tatizo ni wewe mwenyewe. Hivyo ni vyema sana kabla hujaanza kutafuta sababu na watu wa kuwalaumu uakajua chanzo cha tatizo unalopitia.

Embu kumbuka siku moja unapopitia tatizo halafu ukaanza kuwatupia lawama wengine, baada ya muda unakuja kugundua kumbe ni wewe mwenyewe ulisababisha tatizo lile. Ni vyema kabla hujaanza kutupa lawama kwa wengine kwenye jambo linalotokea ukajua chanzo chake kwanza.

Kiitu cha mwisho nataka kukwambia chanzo cha yote yanayoendelea kwenye maosha yako sasa hivi ni wewe mwenyewe. Unajua ni nini ndugu, yanapotokea mambo mazuri tunapenda kuonekana ni sisi tumeyafanya lakini yanapokuwa ni mabaya tunatupia lawama wengine.

Mbona unapofanya vizuri huanzagi kusema sio wewe ni Fulani amesababisha? Kama ukifanya mabaya pekee ndio unatafuta watu wa kuwatupia lawama unapotea kabisa. Watu wenye mafanikio makubwa wanatatua matatizo yao wenyewe bila ya kuwatupia lawama wengine.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading