Muda ni kitu cha Thamani sana, muda ndio umebeba maisha yetu. Kama utakuwa unatumia muda wako kuwasema watu kwa wanayofanya unapoteza sehemu ya maisha yako.

Kama mtu amefanya vibaya njia nzuri ya kumsaidia ni kwenda kumwambia na sio kumsema pembeni. Kama mtu huyu huna uwezo wa kwenda kumweleza makosa yake na unataka kweli kumsaidia tafuta mtu ambaye ataweza kwenda kuzungumza nae. Ukikosa kabisa basi kaa kimya.

Watu wengi tunapoteza muda wetu kuwasema watu vibaya halafu watu tunaowasema hawajui kabisa kama wanasemwa.

Unapoteza muda wako kwenye mambo yasiyo na faida kwako wala kwa wengine.

Kuna msemo unasema kwamba,  hakikisha lolote unalozungumza kuhusu mtu pembeni una uwezo wa kulisema mbele yake.

Mtu mwenye maono makubwa na anaejua anapoelekea hana muda wa kukaa na watu akiwasema vibaya wengine. Tumia muda wako kwenye kutengeneza maono yako yawe kweli.

Tumia muda wako kwenye ndoto zako.

Sijasema watu wakikosea wasiambiwe. Ninasema ni kupoteza muda kumsema mtu pembeni halafu hajui. Na inawezekana hata hilo baya unalomsema nalo hajui kama ni baya.  Kama huna nafasi ya kuweza kumwambia kaa kimya unapoteza muda wako.

Wewe binafsi sidhani kama utafurahia ukikuta kuna kikundi cha watu kinakusema mambo yako. Utafurahia endapo umekosea mtu akakufata na kukwambia njia unayoindea sio nzuri jaribu kubadilika.

Hivyo Rafiki yangu tumia muda wako vizuri. Maisha yako hakuna anaeyawazia kama unavyowaza juu ya wengine. Ndoto zako ni wangapi wanazijua? Inawezekana hata wewe mwenyewe hujaelewa vyema unapoelekea lakini unatumia muda mwingi kuwasema wengine.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading