HATUA YA 185: Vitu Ambavyo Kila Mtu Anaweza Kufanya..

Siku zote kama unafanya kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya hakiwezi kuleta mchango mkubwa kwenye maisha yako. 

Kama unataka matokeo ya tofauti basi achana na mambo uliyozoea kuyafanya.

Watu wengi wanapenda kutoa sababu na kulalamika. 

Kila mtu anaweza kusema lakini ni wachache wanaochukua hatua.

Kila anaweza kufanya biashara lakini sio kila mmoja anaweza kufanya biashara kwa namna ya tofauti kwenye jamii yetu.

Kama unatamani kuona maisha yako yakibadilika hakikisha umeangalia mambo ambayo unayafanya mara kwa mara kama ni watu wa kawaida wanayafanya.

Jaribu kuangalia maisha yako ya kila siku ni vitu vingapi ambavyo unafanya vinaleta tofauti yako na watu wa kawaida?

Kama kila mtu anaweza kuanzisha biashara kama yako wewe umeamua kufannya kitu gani cha tofauti?

Jitofautishe na wengine maisha yako yatakuwa ya tofauti.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/


Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *