HATUA YA 186: Usiwe Mmoja Wao.

jacobmushi
2 Min Read
Usiwe mmoja wao wanaolalamika badala ya kuchukua hatua. Usiwe mmoja wao ambao matatizo yao wenyewe wanatafuta watu wa kuwabebesha badala ya kuyatatua.
Usiwe mmoja wao ambao wanafanya mambo kwa kufuata mkumbo. Usiwe mmoja wao hao ambao wanategemea maisha yao yabadikike wakati hakuna wanachokifanya ili kuyabadili.

 

Ndio rafiki yangu nakwambia usiwe mmoja wa hao wakatishaji tamaa. Usiwe mmoja wa hao wanaoona wivu wenzao wakiendelea badala ya wao kujifunza kwao. Anza kubadilika sasa hakuna kitakachobadilika kama wewe hutabadilika.
Katika kundi la wengi wanaofanya mambo yanayonafanana usikubali kuwa mmoja wao. Amua kufanya mambo ya tofauti. Kama wote wanakaa dukani na kungojea wateja waje anza kufanya tofauti na wao. Anza kufanya wateja waje usiwasubiri. Anza kuhudumia vizuri wateja wako.
Tafuta kitu kinachokutofautisha na wengine. Kama huna tofauti basi wewe umekuwa wa kawaida na watu wenye mafanikio ni wale waliogundua utofauti wao.
Mabadiliko yanaletwa na utofauti. Ukiweza kujitofautisha ndipo unakwenda viwango vingine. Kama wengine wanalalamika magufuli kabana wewe funga mdomo kafanye kazi. Wakati watu wanasema hawana mtaji wewe anza na kile ulichonacho kidogo kidogo hadi ufikie kule unakotaka.
Usikubali kufanya mambo ambayo wengi wanakimbilia. Hii ni kwasababu wengi hukimbilia kufanya vitu virahisi na vinavyowezekana lakini wenye mafanikio wanafanya mambo ambayo watu wa kawaida wanaona hayawezekani.
MAFANIKIO YAKO YAPO KWENYE UTOFAUTI WAKO.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading