HATUA YA 188: Imani Yako itakuponya au Kukuua.

jacobmushi
2 Min Read
Vile ulivyo sasa kunatokana na Imani yako juu ya vitu mbalimbali vilivyokuzunguka. Matokeo mbalimbali unayopata kwenye Maisha yako yanatokana na kile unachokiamini. Ukifanya kazi kwa bidii kuliko wengine halafu moyoni mwako unaamini matajiri ni wachawi kamwe huwezi kuwa tajiri.
Lazima kwanza uanze na kuamini moyoni mwako kwanza kwamba inawezekana ndipo ukija kwenye vitendo vilete matokeo. Kama hujaamini hata ukipambana na vitendo kiasi gani bado hutapata matokeo unayoyataka.
Soma: Badili hali Uliyonayo Sasa Hivi
Anza kuondoa Imani potofu ulizonazo kwenye moyo wako. Imani kwamba ukiwa na pesa nyingi utamsahau Mungu. Imani kwamba wenye pesa ni wabaya, wamedhulumu, na mengine mengi. Fikra zako zikipingana na matendo yako huwezi kupata matokeo unayoyatarajia.
Hakuna kazi ngumu kama kumwondoa mtu kutoka kwenye fikra alizojengewa tangu akiwa mdogo. Kwenye akili yako unaona haiwezekani halafu unaweka vitendo vingi hakuna matokeo yeyote utakayoyaona.
Leo jipe muda utafakari hivi ni kweli unaamini inawezekana? Kuna fikra gani hasi zinazokutesa juu ya vitu ambavyo unavitaka? Anza kwa kubadili fikra zako.
Tengeneza Imani mpya kwenye vitu ambavyo unataka vitokee kwenye Maisha yako. kamwe usipoteze nguvu zako kwenye kitu ambacho moyo wako haujakikubali huwezi kupata matokeo bora.
Moyo wako wako ndio unatakiwa ukupe ruhusa ya kufanya jambo. Moyo wako unaweza kukufanya ushindwe kufanikiwa kwasababu ya vile ulivyovijaza ndani yake. Safisha kila Imani potofu uanze upya.
UNACHOKIAMINI NDIO KIMEKUFANYA UWE HIVYO ULIVYO SASA.
#USIISHIE NJIANI
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading