Maisha yako yapo mikononi mwako, ukishindwa kupangilia siku yako vizuri unapanga kuipoteza. Ili uweze kuwa na juma lenye uzalishaji bora ni vyema ukawa na ratiba yako ya kila wiki. Jua ni vitu gani vya muhimu ambavyo utakwenda kuvifanya kabla wiki haijaanza.

Pangilia Wiki Yako Kabla Hujaianza.
Kwa kawaida wote siku ya Jumapili tunaitumia kama mwisho wa wiki na Jumatatu mwanzo wa wiki. Ni vyema kabla haijafika siku ya jumatatu uwe umeshaweka mpango ni kwa jinsi gani unakwenda kuwa na wiki ya uzalishaji na matokeo bora. Kulingana na maono yako na kile ambacho unafanya kila siku weka malengo ya vitu ambavyo unataka kuvitimiza ndani ya wiki husika. Gawanya malengo yako kwa siku moja moja hadi mwisho wa wiki. Jambo hili unatakiwa ufanye kila siku ya jumapili. Hii itakupa mwangaza wa kujua unapokwenda na kungalia vyema maendeleo yako.

Amka Asubuhi na Mapema Kila Siku.
Ili uweze kuwa na siku bora amka mapema sana kwa kawaida muda wa mzuri wa kuamka ni saa kumi na moja asubuhi, ila mwingine anaweza kuamka mapema Zaidi ya hapo. Muda huu unatakiwa uutumie kupangilia siku yako na kufanya yale mambo ya muhimu sana. Tenga muda wa kuomba Mungu angalau dakika 20.  Muda huu unatakiwa usome kitabu angalau kurasa kadhaa kulingana na uwezo wako wa kusoma. Mwingine anaweza kusoma sura moja mwingine kurasa kumi. Muda huu utumie kufanya mazoezi, unapoamka asubuhi na kufanya mazoezi unajitengenezea nafasi ya kufanya mambo kwa ufanisi mkubwa. Kama utakua ni lisaa limoja umepata asubuhi gawanya kwa dakika 20 kwa kila unachokifanya. Omba Mungu, Soma kitabu, Pitia maono yako na kupangalia siku, Fanya mazoezi.
Fanya Mambo Magumu Kwanza.
Muda wa asubuhi ndio muda ambao akili yako ina nguvu na una uwezo wa kufanya mambo makubwa ziadi. Muda huu ndio wa kutumia kufanya yale mambo ambayo ni magumu na yanayokusumbua. Kama utakumbuka ukiwa shuleni somo la Hesabu likifundishwa asubuhi wengi tulikuwa tunapendelea Zaidi kuliko mchana. Mara nyingi mchana wengi tulikuwa tunasinzia.  Asubuhi ndio wakati akili yako inafanya kazi kwa haraka na inakuwa bado haijachoka.


#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading