Mojawapo ya vitu ambavyo havitaweza kubadilishwa ni vile ambavyo aliviumba Mungu. Lakini kila alichogundua mwanadamu unaweza kufikiri namna ya kukiboresha.

Mwanadamu ukisema umuongezee kiungo kingine unaharibu mfumo mzima au hawezi kuwa sawa na wanadamu wengine.
Huwezi kubadili chochote kinachotokana na asili. Waliojaribu kutuletea vitu ambavyo ni vya asili wakajaribu kurekebisha vinaleta madhara makubwa kwenye Maisha ya wanadamu.
Kama kuna kitu unataka kukibadilisha angalia ambacho amegundua mwanadamu mwenzako unaweza kurekebisha lakini sio kinachotokana na asili.

Mwanadamu alikuwepo tangu miaka yote hiyo alichoweza kubadili ni mavazi na sehemu ya kuishi lakini sio katika mwili wake.
Ninasema haya kwa wote wale wanaojaribu kwa namna yeyote kujibadilisha iwe ni sura au jinsia lazima utaleta uharibifu.
Mti tokea mwanzo ulikua unaitwa mti na hakujawahi kutokea mti toleo la pili.

Mwanadamu tokea anaumbwa ni mwanadamu hakujawahi kutokea wanadamu toleo jipya.

Kama unataka kupotea katika historia ya dunia jaribu kubadilisha asili. Hutaweza kazi ya Mungu alifanya mara moja na hajawahi kuurudia.
Mungu pekee ndio vitu vyake havinaga toleo jipya. Kama umejikuta kwa namna moja ama nyingine unatamani kubadili uumbaji wa Mungu aisee unakwenda kupotea haraka sana.

Chochote kile kilichogunduliwa na mwanadamu mara nyingi hakina uwezo wa kujizalisha chenyewe lazima mwanadamu aje aweke mkono wake tena ili atengeneze kingine. Lakini alivyoumba Mungu vina uwezo wa kujizalisha na kuongezeka vyenyewe miaka na miaka.

Magonjwa mengi tuliyonayo yanasabishwa na kuingiza ndani ya miili yetu vitu ambavyo havitokani na asili ya uumbaji wa Mungu.

 KUMBUKA: Huwezi kubadili asili. Unaweza kubadili alichovumbua mwanadamu pekee yake. Jitazame ni vitu vingapi ambavyo umebadili kwenye mwili wako ambavyo havikutakiwa kubadilika uache mara moja.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading