Kuna dharura zinajitokeza wakati upo kwenye shughuli zako na kuna dharura zinatokea na wewe upo upo tu hujui cha kufanya.
Kama utashindwa kutofautisha vitu vya dharura na vitu vya muhimu kwenye Maisha yako utajikuta unapoteza mwelekeo wa Maisha yako.

Vitu vya dharura ni vitu vile ambavyo mara nyingi vinajitokeza kwenye ratiba yako na hukuwa umevipangilia. Mara nyingi vitu hivi vinakuwa havipo katika mpango wako na huna uwezo wa kuamua vitokee au visitokee.

Ukishindwa kutambua vitu hivi unaweza kujikuta unafanya mambo ambayo hayana mchango wowote kwenye baadae yako. kabla hujaamua kufanya maamuzi hakikisha umetambua dharura iliyojitokeza ni ya muhimu au sio ya muhimu. Njia rahisi ya kutambua ni kwa kufikiri, jiulize hii dharura nisipoifanyia kazi italeta matokeo gani? Kama kuna matokeo mabaya yatatokeo basi ifanye lakini kama hakuna madhara yeyote dharura hiyo siyo ya muhimu.

Kuna mambo mengine yanakuja kuwa dharura kwasababu hatukuyafanyia kazi wakati wake uliokuwa unahitaji.
Maisha ya Dharura.
Usikubali kabisa Maisha yako yakawa ni ya dharura wewe huna ratiba ya Maisha yako binafsi unategeme jambo litakalotoke mbele yako ndio unafanya.

Wakitokea marafiki wanamipango yao wanakubeba. Likitokea tukio popote wewe upo. Huna ratiba ya Maisha yako binafsi. Ukiulizwa kesho utakuwa wapi huelewi.

Kuishi Maisha ya dharura kunasababishwa na watu kutokuwa na maono na malengo. Kama hujui unapoelekea chochote kitakuchukua. Kama huna ratiba zako mwenyewe ratiba za wengine zitakuchukua.
Usipopanga ratiba zako utaingia kwenye ratiba za wengine.

Hakikisha unajua unapoelekea, kabla hujaianza siku yako ipangilie jua vitu vya muhimu unavyokwenda kuvifanya siku hiyo. Kama utashindwa kupangilia siku yako utaingia kwenye mipango ya watu wengine.
Hujawahi kukutana na watu ambao ukiwauliza wana muda utoke nao out siku zote wao hua na muda. Hakuna hata siku moja wamesema ratiba imebana.

USIKUBALI KUWA MTU ANAEISHI MAISHA YASIYO NA VIPAUMBELE NA MPANGILIO.
 Kama unafikiri Una muda mwingi wa ziada basi fanya vitu hivi.
Soma vitabu.
Fanya mazoezi.
Sikiliza Audio Books.
Jifunze vitu vipya kwenye mtandao wa Youtube.
Andika vile vitu unavyovipenda na unatamani wengine wajue.
Tembelea Blogu hii kujifunza kila siku.


#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading