HATUA YA 193: Ukitaka Kuaminika…

Ukitaka kuaminika usiwe mtu wa kubadilika badilika kutokana na mazingira uliyopo au unapokuwa na watu wa aina Fulani. Ukitaka kuaminika kuwa wewe siku zote. Ukitaka kuaminika kuwa mtu ambaye unatabirika yaani watu wakikuacha mahali wanaamini hutabadili tabia.

Unayafahamu maji? Maji ukiyaweka kwenye ndoo yatakaa na yatabeba umbo la ndoo. Vilevile maji ukiyaweka kwenye mfuko yatakaa na yatabeba umbo la karatasi. Maji vile vile ukiyaweka kwenye chombo cha rangi yatachukua pia ile rangi ya chombo.
Sasa wewe usiwe na sifa za maji watu watashindwa kukuamini maana huna msimamo. Hujulikani hasa tabia zako ni zipi. Ukishakuwa na sifa za maji watu wanaanza kukuogopa kwasababu unaweza kufanya kitu cha ajabu sana.
Unajua maji ukiyaweka kwenye ndoo yatakaa ukiyamwaga chini yatasambaa kila mahali. Sasa wewe ukiwa na sifa hizi za maji unakosa mtu wa kukuamini au kukuacha mahali peke yako maana unaweza kuharibu mambo.


Mojawapo ya watu ambao wanaleta shida kwenye hii dunia ni watu wenye sifa za maji. Kuwa mtu mwenye msimamo na tabia zako. Usiwe mtu ambae unaigiza tabia ukiwa na wazazi ni mtu mwingine kabisa hata unavyoongea. Ukiwa na marafiki ni mtu mwingine kabisa. Ukiwa na mpenzi wako ni mtu mwingine kabisa.
Sijasema uwe mtu ambae unakuwa wazi kwa kila unalofanya na kwa kila mtu bali uwe na misimamo ambayo inaeleweka. Mtu akitaka kukuelezea ataje zile tabia ambazo ukikaa na kila mtu zinaonekana.
Haitakiwi mtu aweze kujua vyema mambo yako lakini unatakiwa uwe na tabia zisizobadilika kutokana na mazingira. Yaani hata uwe wapi bado tabia zako na vitu ulivyoamua kuvisimamia vitakua ni vile vile. Tuseme ukikaa na wazazi au watu ambao wanakuamini unafanya matendo ya uaminifu lakini ukiwa mbali nao unafanya vitu ambavyo wakija kukuona bila ya wewe kujua wanaweza kufunga macho.
Mfano rahisi ni wanafunzi wanaoshi mbali na nyumbani, unakuta tabia zako ukiwa chuoni ni tofauti kabisa na tabia zako ukiwa mtaani kwenu. Ukichukua mtu pale mtaani kwenu aeleze sifa zako zinakua ni sifa tofauti kabisa na zile ambazo ukiwa shuleni zinaonekana.
KUMBUKA: Uadilifu ndio msingi wa mafanikio. Ukiukosa huwezi kuwa na mafanikio sehemu yeyote. Utayumba kila kona sio kwenye mahusiano,ajira,  fedha hata biashara.


#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.
jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading