HATUA YA 195: Kizazi cha Kuona Kwanza na Kuamini.

jacobmushi
2 Min Read
Tupo kwenye kipindi ambacho watu wake hwaamini tena mpaka waone. Kizazi ambacho hakiamini matendo ya Imani mpaka kione kwa macho ya damu na nyama. Tuna watu wengi sana ambao hawawezi kuamini chochote unachowaambia bila ya kuona ishara ya papo kwa papo.

Kama huwezi kujenga Imani kwanza ndipo uone matokeo utaishia kudanganywa kwenye mambo mengi ya Maisha yako. Kama Imani yako imejengwa katika misingi ya kuona ishara kwanza ndipo ukubaliane na jambo huwezi kufikia mafanikio.


Tukianza kuangalia katika Biblia watu wengi ambao walipokea uponyaji wao walianza kuamini kwanza ndipo wakapona. Ndio ni kweli kilichowafanya waamini ni watu wengine waliotangulia kuponywa pamoja na habari nyingi walizozisikia. Lakini wengi walipokea uponyaji kwa kitu cha ziada walichokifanya sio kwa kusikia ishara tu.
Kwa mfano kipofu ambaye alikwenda kwa Yesu ilia one ni baada ya kusikia ishara nyingi kwamba anaponya. Lakini akapakwa matope machoni kisha akaambiwa akanawe. Kwa kizazi cha sasa umwambie mtu muujiza wake upo hivo hawezi kukuelewa kabisa.
Ili mtu aamini ni hadi aone kile alichozoea kukiona lakini Imani ni tofauti lazima uanze kujenga picha yako binafsi ndani. Iamini picha hiyo na uifanyie kazi ndipo itatokea. Ili mtu aamini umefanikiwa mpaka aone na akupime kwa vitu ambavyo wengine wanavyo ndipo atasema umefanikiwa.
KUMBUKA:
Ukweli kuhusu mambo yote yanayotokea kwenye ulimwengu huu ni lazima uanze kuona ndani ya ufahamu wako na uamini kile ulichokiona kisha uanze kukifanyia kazi mpaka kitokee. Lazima uanze kuamini ndipo matokeo yafuate kama unataka matokeo kwanza ndipo uamini utasubiri sana.


#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading