Kuku anapotaka kutaga kwa mara yake ya kwanza lazima atafute sehemu nzuri na aitengeneze ili aweze kutaga vizuri. Kwa bahati mbaya sana kuku hana akili hivyo anaweza kujitafutia sehemu yeyote tu hata nje ya banda lake. Ila kwa mfugaji anaejua kitu anafanya lazima awaandalie kuku wake mazingira ya kutaga pale wanapohitaji kutaga.

Kipindi Fulani kuku wetu hatukuwa na utaratibu wa kuwaandalia mazingira ya kutaga hivyo walikuwa wanajitafutia wenyewe. Kuna kuku walikua hawatagi kabisa na wamefikia umri wa kutaga sasa katika kufuatilia tukaja kugundua kuna mmoja alikua anataga kichakani na mwininge kwa jiarani.
Nimeanza na mfano wa kuku ili tuelewane vizuri. Kuna mambo ambayo hayatokei yenyewe kwenye Maisha kama hujaandaa mazingira. Na bahati mbaya sana yakitokea yanaweza yakatokea sehemu ambayo haijaandaliwa vizuri na ukawa umeyapoteza.


Andaa mazingira kwa ajili ya fursa zinazoweza kutokea kwenye biashara yako au kile unachokifanya.
Unafikiri yale mayai yanayotagwa kwa jirani unaweza kuyapata kweli? Au yale ya kichakani mara nyingi yanaweza kuliwa na nyoka au yakaharibiwa na vitu vingine. Hivyo ndivyo wakati mwingine fursa zako zinapotea kwa kushindwa kuandaa mazingira.
Ukijua vizuri unachokifanya na unapokwenda utaweza kuelewa sehemu gani hasa uzitengeneze na kuziandaa kwa ajili ya fursa zinazoweza kujitokeza. Unaweza kujua vyema unachokifanya kwa kujifunza kila siku.
Ili usije kuwa mtu wa kusema ningejua, ningejua nyingi andaa mazingira. Kuna fursa nyingi zitakupita mbele yako kwasababu tu hukujiandaa. Jitengeneze vya kutosha, muda ambao unao wa ziada utumie kujifunza vitu vipya. Kila unachojifunza kinaweza kuja kuwa msaada kwa namna moja ama nyingine huko mbeleni.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading