Ukikosa vipaumbele huwezi kujua ni nani anastahili muda wako Zaidi ya wengine hivyo utakua unapoteza muda hata kwa watu wasio wa muhimu.

 

Ukikosa vipaumbele huwezi kujua  kipi ni cha muhimu Zaidi ya kingine hivyo utakuwa unafanya vitu hovyo hovyo tu.
Ukikosa Vipaumbele utachukuliwa na kila kinachokuja mbele yako itakuwa ngumu sana kwako kufanya uchaguzi.
Soma: Kitu gani Unakipa Muda zaidi?
Ukikosa Vipaumbele Maisha yako utakuwa umeyapoteza itakuwa ngumu sana kufikia vile unavyovitaka.
Maisha Yako YanaTafsiriwa na vile vitu unavyovipa vipaumbele Zaidi, hivyo kama huna vipaumbele umeyakosa Maisha yako. Chanzo kikuu cha watu kukosa vipaumbele ni kutokujua wanapokwenda, kutokujua wanachokitaka.
Ili uweze kuwa na vipaumbele lazima ujue unakotaka kufika na uwe na malengo na mipango ya kufika kule uendako. Lazima uwe una watu unaowapa vipaumbele kwasababu ni wa muhimu kwako na wana mchango mkubwa wa kule unapoelekea.
Maisha yako yanahitaji kuwa na vipaumbele kulingana na ndoto na maono yako, vile vitu unavyotaka vitokee kwenye Maisha yako ndio uwe unavipa nafasi kila siku ya kuvifanyia kazi hadi viwe kweli. Wale watu ambao utakuwa nao hadi mwisho wa safari yako hapa duniani ni watu wa muhimu sana hivyo usiwasahau.
Kamwe usikubali kuwa mtu ambaye hana vipaumbele rafiki, usiwe mtu ambaye wewe kila ukihitajika na mtu yeyote unakuwa upo na muda hata kwenye mambi yasiyo ya msingi. Usiwe mtu ambaye mara zote una nafasi huna jambo lolote unalolifanyia kazi kila siku. Usiwe mtu ambae huna kitu kinachoumiza akili yako kwamba utafanyaje kitokee.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading