HATUA YA 199: Wasikilize Lakini Amua Wewe.

Kwenye vitu tunavyovifanya kila siku tunakutana na maoni ya wengine kila siku. Jambo la muhimu ni kwamba usikatae kupokea maoni ya watu. Kitu unachotakiwa ni kuyachuja na kuchagua yale ambayo unaona yanafaa kule unapoelekea.

Usiruhusu watu wakufanyie maamuzi maana wewe ndie unajua unapoelekea. Usiwape wengine madaraka ya kuamua wewe uwe na baadae ya aina gani. Beba Maisha yako mwenyewe. Haijalishi wanakupa msaada kiasi gani hiyo siyo sababu ya wao kumiliki Maisha yako.

Kama ukiona kuna maamuzi unataka kufanya halafu kuna watu ukiwatazama unaanza kupata wasiwasi kwamba watakuelewaje basi ujue huna umiliki wa Maisha yako. Kuna hatua unatakiwa ufike ambazo uwe na uwezo wa kuamua sio kuomba ruhusa Zaidi unachofanya ni kutoa taarifa sio kuomba ruhusa.

Soma: WEWE NI MSHINDI

Ukifikia kiwango cha kubeba umiliki wa Maisha yako yote mwenyewe unakuwa huna wa kumlalamikia wala kumlaumu. Unakuwa unawajibika kwa maamuzi yeyote utakayochukua kwenye Maisha yako yawe mabaya au mazuri.

Kama huelewi unapokwenda siku zote unakuwa tegemezi kwa wengine kwa kiasi kikubwa na hivyo wale unaowategemea wanakuwa na maamuzi makubwa kwenye Maisha yako. unakuwa huna uwezo wa kuamua mambo makubwa mpaka ukaombe ruhusa. Na kwenye kuomba ruhusa kuna kukataliwa au kupewa.

Mambo ya Kufanya ili Umiliki Maisha Yako:

Jua Kusudi lako

Jua Unapotaka Kufika.

Kuwa na Ndoto Kubwa.

Tafuta Mtu wa Kukuongoza na Kukushauri.

Anza kufanyia kazi ndoto zako hadi zitimie.

MAISHA NI YAKO BEBA UMILIKI, JUA UNAPOKWENDA.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

This entry was posted in HATUA ZA MAFANIKIO on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *