Nunua kitu Kwasababu unakihitaji sio kwa ajili ya kuwaonyesha wengine kwamba una uwezo wa kipesa.

Tatizo kubwa linalotusumbua ni kwamba tunafanya mambo ili watu watuone. Mtu ananunua mavazi ya gharama sio Kwasababu anayahitaji bali ni ili watu wajue ana uwezo wa kipesa.

Mwingine ananunua gari jipya ili watu waone sio Kwasababu ya mahitaji yake. Ukiwa mtu wa hivyo utakua mtumwa sana wa kuwaonyesha wengine.

Kama mtu analipwa mshahara wa laki sita anatamani watu waone anavaa mavazi yanayoendana na mshahara wake, nyumba anayoishi iendane na mshahara wake. Sehemu anazotembelea ziendane na mshahara wake. Mwisho wa siku anajikuta mshahara hautoshi na ana madeni kibao.

Suluhisho:

Kama unanunua kitu kwa ajili ya kuwaonyesha wengine unapotea ndugu yangu. Usinunue IPhone 7 ili watu wakuone uko juu. Nunua Kwasababu Unahitaji IPhone 7 kwa matumizi yako.

Chochote unachotaka kufanya leo usiache kujiuliza kama ni kweli unakihitaji au unataka watu waone unaenda na mtindo mpya.

Usipokubali kunisikiliza mwisho wa siku madeni yatakua ni yako. Mshahara usipotosha utateseka wewe mwenyewe.

Jaribu kuishi chini ya kipato chako ili uweze kujitengenezea uhuru wa kipato.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author | Trainer | Entrepreneur

Simu: 0654 726 668 |0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Facebook:  Jacob Mushi 

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading