Leo ni siku ya 200 mfululizo tangu nimeanza kuandika. Unaweza kufikiri ni kitu rahisi lakini sio kitu rahisi maana ili uandike lazima ujilazimishe kufikiri sana. Sasa kama mtu ni mvivu kufikiri hawezi kuandika kila siku.

Lakini ni kwambie siri iliyopo nyuma ya hizi hatua 200? Wakati naanza nilifika hatua kama ya 50 hivi wakajitokeza watu wengi sana waliokuwa wanapinga. Wengine wakaniambia hizi hatua mbona ni nyingi sana? Ungeandika kama 20 tu. Sasa nikawa najiuliza moyoni hivi mtu anakuambia hivi anajua kweli dhumuni la wewe kuanza kuandika?
Mwingine akasema unapoteza muda na hayo mahatua yako katafute kitu kingine cha kufanya.  Nikasema sasa kama ninachokifanya kuna wengi wanasema kinawasaidia halafu yeye anasema napoteza muda yeye ni nani?
Mwingine akasema usiwe unatuma haya mahatua yako kwenye group letu. Tuma vitu vingine lakini sio hzio hatua. Nikajisemea moyoni hizi hatua zina shida gani?

Mwisho wa siku nikatafakari wote hao waliokuwa wananipinga na kunishauri jinsi ya kufanya kazi yangu kwanza hakuna mwandishi hata mmoja. Pili hakuna hata mmoja ambaye amewahi kununua japo kitabu au hata kujiunga na semina ninazoendesha. Nikasema sasa hawa watu wanapataje nguvu ya kunishauri? Wanajua kweli ninapokwenda? Mbona wananiambia niache ninachokifanya?
Mwisho wa siku nikasema ngoja niwatazame tu wale ninaowaandikia wakijitokeza watakaonishauri vizuri nitawasikiliza lakini sio wanaosema niache kuandika. Pia angalau anaenishauri awe anafanya kitu kama hiki ninachokifanya hapo kidogo ninaweza kusikiliza ushauri wake kwa makini Zaidi.
Sio vibaya mtu mwingine akikushauri lakini unachotakiwa kupima ni ushauri anaokupa una lengo gani? Kama lengo ni wewe uache unachokifanya ukafanye kingine huyo mtu ni hatari sana. Hasa kama unachokifanya ndio kitu ulichochagua kufanya Maisha yako yote.
Rafiki yangu ni kwamba usione watu wanafanya vitu ukafikiri hakuna changamoto hizo nilizosema ni chache tu kati ya ninazopitia. Chochote unachokifanya kuna changamoto nyingi utazipitia sana. Nyingi zinakuja kama kukurudisha nyuma. Nyingi zinakuja kama kukuzuia usifanye kile ulichochagua kufanya.
Kama utakosea na kuzitazama changamoto kwa mtazamo mbaya utajikuta unaishia njiani. Unachotakiwa kupima changamoto za kukatishwa tamaa zinakuja kwa lengo gani. Kama ni kukurudisha nyuma basi usije ukaziruhusu zinachukua nafasi.
Ndio maana ninashauri uwe unapitia maono yako mara kwa mara. Uwe unasome ndoto zako angalau kila siku. Uwe unaziandika tena upya angalau kila siku. Unapofanya hivi unazifanya zikae katika ubongo wako wa ndani hivyo sio rahisi uzisahau. Hata wakitokea wakatishaji tamaa utakuwa na nguvu kubwa ndani yako ya kuvumilia.
Kitu cha Kufanya:
Jua Vizuri unapokwenda.
Ukijua vizuri unapokwenda huwezi kuyumbishwa na wasiojua unapokwenda wanapokuja kukushauri mahali pengine pa kwenda. Wengi wanaacha wanachokifanya kwasababu hawakuwa na uhakika wa kutosha na safari waliomua kuiendea. Anapotokea mtu mwenye nguvu kubwa juu yako akakushauri kitu kingine cha kufanya unajikuta unaona kile unachokifanya hakina nguvu kama ulichoshauriwa.
Kuwa na Msimamo.
Kama huna msimamo utayumbishwa na misimamo ya wengine. Unasimamia kitu gani? Kitu gani hasa kinakusukuma wewe kufanya hicho ulichoamua kufanya?
Lipa gharama.
Amua kulipa gharama ili ufike kule unakotaka. Bila ya kulipa gharama huwezi kupata matokeo yale unayotaka. Gharama ndio kipimo cha thamani ya kile unachokifanya. Kiwango cha gharama ndio kiwango cha mafanikio yako.
Leo  ninaomba jambo moja kwako wewe msomaji wangu wa Makala hizi. Naomba unipe ushuda hadi leo siku ya 200 umejifunza kitu gani kwenye hatua hizi. Kuna matokeo gani umeyapata kwenye Maisha yako baada ya kusoma Makala hizi. Nitumie kwenye email yangu jacob@jacobmushi.com
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading