Kanuni ya Umaskini ni kutumia Zaidi ya unachozalisha. Kama unataka kubakia kuwa maskini endelea kuwa na matumizi makubwa kupita uwezo wako wa kuzalisha. Kama wewe ni mkulima ukizoea kula Zaidi ya unachozalisha mwisho wa siku utakula na mbegu inayokuzalishia. Kama wewe ni mfanyabiashara ukizoea kutumia Zaidi ya unachopata utaanza kula mtaji.

Kanuni ya mafanikio inasema kama unataka kutumia Zaidi basi zalisha Zaidi. Hivyo chochote kile unachokitaka kama kimezidi kipato chako unachotakiwa ni kuongeza uwezo wako wa kupata kipato. Kama wewe unataka kula mayai matatu kila siku halafu una kuku mmoja utakuwa unajidanganya bure kwasababu kuku anataga yai moja tu kwa siku. Njia pekee ya kuweza kula mayai matatu kila siku kwa kutegemea kuku ni kuongeza idadi ya kuku. Na sio uwe na kuku watatu pekee kwasababu wanaweza wasitage kila siku. Hivyo pia kwenye vingine vyote unavyofanya ukitaka Zaidi ongeza uwezo wako wa kupata.
Maisha yako yataendelea kuwa magumu Zaidi kama utakuwa unatumia Zaidi ya unavyozalisha. Kwasababu kila mmoja anatamani aonekane ana maendeleo basi hakuna haja ya kutengeneza picha ya nje ya uongo kwa kununua vitu ambavyo havijafikia uwezo wako. Badala yake angalia ni wapi unapoweza kugusa ili uongeze uzalishaji wako.
Kama unaweza kuuza bidhaa yako kwa wateja watano kwa siku basi ongeza bidii mara tatu yake hakikisha umeweza kuwafikia wateja 15 kwa siku.
Kama umeajiriwa basi tafuta muda ambao unaweza kuutumia kutengeneza kipato cha ziada.
Kama unasoma chuo hakikisha unajitengenezea njia za kutengeneza kipato ukiwa hapo chuoni kwa kutumia zile pesa unazopata za mkopo au unazotumiwa nyumbani.
Hakuna namna nyingine unayoweza kufikia unachokitaka kama hutakubali kuzalisha Zaidi ya unavyotumia.
Chochote unachokitaka utakipata kwa kuweka bidii kubwa na kutokukata tamaa. Yale Maisha unayoyatamani kuishi usianze kuishi kwa kuigiza fanya kazi kwa bidii uyapate kihalali. Ni ujinga kabisa kuwaonyesha watu una Maisha mazuri wakati ndani unateseka.
UKITAKA KUTUMIA ZAIDI ZALISHA ZAIDI. USILE MBEGU.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading