Sehemu uliyoizoea ndio inafanya uwe na hali uliyonayo sasa hivi. Kama hapo ulipo unapata kila unachokitaka jiulize je utaendelea kupata unachokitaka kwa muda gani? Kama ukiona hakuna  muda mrefu hatua unayopaswa kuchukua ni kuondoka.

Nyumbani kwako kunaweza kuwa ni kazini kwako pamoja na mshahara unaopokea. Inawezekana unadanganyika na mshahara unaopokea ukafikiri maisha yatakuwa hivyo siku zote. Ukajisahau kwamba siku yeyote unaweza kufukuzwa kazi. Ukabaki unatazama vile vitu kazi imekufanyia ukasahau unahitajika kusonga mbele zaidi.
Nyumbani kwani inawezekana ni faida uliyozoea kuipata kwenye biashara yako. usikubali kubaki nayo kwani hujui ni siku gani mambo yataakubadilikia. Usikubali kupata faraja kisha ukajisahau hasa kwenye vitu visivyodumu.
Umeshaona mtu amekaa kwao hadi amesahau kwamba anatakiwa aoe au aolewe. Hii ni kwasababu nyumbani anapata kila anachohitaji hivyo hana muda wa kutafakari maisha yake mwenyewe. Mtu anajisahau kwamba yale maisha sio yake ni ya wazazi wake.
Usikubali uzoee hali yeyote ambayo sio ya kudumu kwenye maisha yako itakuja kukuumiza.
Bahati mbaya sana kwenye safafiri ya mafanikio wengi hatujengi nyumba za kudumu inakuwa ni vibanda vya kusitiria kwa muda. Usijisahau ukaanza kuishi kwenye kibanda. Bomoa kibanda uendelee na safari.

#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading