Kama kuna mtu  kila anachosema au anachotaka unaitika ndio, bila kuangalia kipo kwenye utaratibu au hakipo,  kitaathiri ratiba zako au maisha yako au lah. Huyo mtu ameyadhibiti maisha yako.

Kama unasema ndio ili kumridhisha mtu na moyo unaumia kwasababu tu ya kitu unachokitegemea kwake huna umiliki na maisha yako.
Usikubali kuwa na maisha ambayo yanategemea sehemu moja kiasi kwamba unakuwa huna maamuzi ya mwisho kwenye maisha yako.
Haiwezekani upo nyumbani unapata chakula cha usiku na familia halafu mtu mmoja anapiga simu bila hata ya kukuomba anasema njoo ofisini kuna dharura.  Unatakiwa ufikie mahali ufanye jambo kwa kupenda na sio kwasababu fulani amesema.
Kama unafanya kwasababu ukikataa utapoteza kazi yako huo ni utumwa. Kama kuna mambo unaogopa kusema hapana kwasababu tu “bosi atanifukuza kazi” huo ni utumwa rafiki yangu. Haijalishi unalipwa sh ngapi.
Fanya mpango uondoke hapo. Tafuta biashara anza kwa muda wako wa ziada. Ipo siku utaniambia umeupata uhuru wako.
Jiunge na USIISHIE NJIANI PROGRAM sasa ili uanze safari ya kuufikia uhuru wako.  Wasiliana nami kwa  0654726668 nikupe utaratibu.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading