HATUA ZA MAFANIKIO

HATUA YA 204: Kama Watu Hawa Wameisha Kuwa Mmoja Wao.

on

Ulishafika mahali ukaona labda dunia haina tena watu wema?
Ulishatendwa kiasi kwamba ukahisi duniani watu waaminifu hakuna hata mmoja?
Watu wamekufanyia mabaya kiasi kwamba ukafikiri duniani sio mahala pa kuishi tena..

Embu angalia kwa makini,  bado kuna mtu mmoja hujamtazama vizuri.  Mtu huyo ni wewe,  jiangalie wewe hizo sifa unazozitafuta unazo?
Embu kuwa mmoja wao hao waaminifu!
Jaribu basi kuwa mmoja wa hao watendao wema!
Onyesha upendo kwa wengine hata kama wote wanaonyesha chuki.

Kamwe usikubali kuwa mmoja wa hao unaodhani ni wabaya tu wamebakia duniani.
Ukilaumu na kusema dunia ya sasa kumpata mtu mwaminifu ni ngumu ukumbuke bado na wewe upo duniani hivyo na wewe sio mwaminifu.

Kuwa mmoja wao,  watu wanaotafuta waaminifu watakukuta.
Kama unafikiri Watanzania ni wavivu hawapendi kusoma vitabu embu anza wewe kusoma achana na hao wengi?

CHOCHOTE UNACHOKITAKA KINAANZA NA WEWE.

#USIISHIE NJIANI

Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.

Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

About jacobmushi

Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *