Siku hizi tumefikia sehemu ambayo kila mmoja anaweza kuonyesha kile anachokifanya kwenye mitandao ya kijamii. Hii imefikia hadi watu kuonyesha tabia zao na pia jinsi wanavyoishi.  Sasa kwasababu ni rahisi sana kuweka picha nzuri akiwa anakula, akiwa hoteli ya ghali, akiwa na furaha sana na mpenzi wake, wewe mtazamaji wa picha ile utaona kama Maisha yao yote yako hivyo.

Ulishawahi kuangalia movie nzuri ukatamani Maisha yote yangekuwa kama kwenye movie? Hivi ndivyo Maisha ya kwenye mtandao yalivyo. Usije ukaona wewe huna Maisha kwasababu ya picha uloziona watu wameweka kwenye mitandao. Ile ni sehemu tu ya Maisha yao. Kuna mengi sana yanaendelea hawayaweki. Kuna magumu wanapitia hawayaweki.

Kwa kawaida wengi unaweza kuona wameweka picha wakiwa na furaha sana wanapata lunch ukafikiri Maisha yao yote yako hivyo. Wakati mwingine unaweza kujitazama ukasema natamani Maisha ya kina Fulani kwenye mtandao. Sasa unasahau kwamba hata wao huwa wanapishana kauli kama wewe. Unasahau kuna nyakati ngumu pia wanapitia sema tu hawaziweki kwenye mitandao.

Ungeweza kufunuliwa japo kwa sekunde kadhaa Maisha halisi ya watu uliozoea kuwaona mtandaoni hutakaa ujaribu kutamani Maisha yao. Sisemi kwamba wote wana Maisha mengine la hasha ila wengi wao ni waigizaji. Pia wengi hatupendi kuonyesha wakati tunatafuta pesa tunapenda kuonyesha wakati tunatumia.

Ukivutiwa na matumizi ya watu jaribu kutamani kuona wanavyotafuta pesa zao.

Usipende kuishi Maisha ya picha maana kuna siku utashindwa kuficha yale yaliyokuwa yanaendelea. Usitamani kila unachokiona mtandaoni unaweza kuona Maisha uliyonayo hayafai lakini ukipewa unayoyatamani utayakimbia. Unaweza kupendezwa na mahusiano ya wengine kumbe umeona nje tu hujui ndani wanaishi vipi.

TENGENEZA AINA YA MAISHA UNAYOYATAKA YAFANYIE KAZI HADI YATOKEE USIIGIZE.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading