Inawezekana Umekuwa Mtumwa wa madeni na hayaishi kila siku unajikuta unatengeneza madeni mapya. Suluhisho sio kuwa na pesa nyingi bali ni kuwa na nidhamu. Kwasababu hata ukiwa na pesa nyingi kama una tabia inayokuingiza kwenye madeni utajikuta unaendelea nayo kila wakati.

Usinunue kitu chochote ambacho Hukupanga.
Kitu chochote unachokutana nacho njiani kiwe kizuri kiasi gani, kama hujapanga kukinunua usikinunue hata kama una pesa mfukoni. Ukweli ni kwamba kama hicho kitu ni cha muhimu sana basi ungekuwa umekiwekea mpango wa kukinunua na pesa yake ingekuwepo.
Usijidanganye na wala usikubali kudanganywa kwamba hautakipata tena kitu hicho, mara nyingi hizo ni lugha za biashara na hazina ukweli wowote.
Usikubali kuchukua kitu na muuzaji akulazimishe uje ulipie siku nyingine, unaingia kwenye jukumu la kuitafuta pesa ambayo haikuwepo kwenye ratiba. Kama kitu huna uwezo wa kukilipia siku hiyo, na huwezi kwenda kutafuta pesa kwanza basi hicho kitu hukihitaji.
Usiwe mtu wa Kupenda Kuonekana Una pesa.
Kuna wakati unanunua kitu sio kwasababu una kipenda bali ni ili tu watu wasikuone wewe ni mbahili. Ili watu waone una pesa nyingi. Ili watu waone wewe sio mchovu. Sasa hapo mtu unaweza kutumia pesa zilizokuwa na kazi nyingine kabisa ukanunua tu kitu kilichokuja mbele yako mwisho wa siku unaondoka ukiwa umejibebesha madeni ya kwenda kulipia.
Haina maana yeyote wewe kuonekana una pesa lakini kwa ndani una mizigo ya madeni inayokusumbua. Haina maana yeyote ya wewe kubeba vitu vya thamani kubwa halafu kumbe ni vya mkopo. Unaowaridhisha hawana chochote wanachoongeza kwenye Maisha yako.
Ishi kwa ratiba na mipango kama kitu hujawahi kukipangilia kununua basi kinaweza kusubiri maana kingekuwa cha muhimu ungekipangilia na kukitafutia pesa yake.
MADENI NI UKOSEFU WA NIDHAMU YA FEDHA.
#USIISHIE NJIANI

Usiache kusoma Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading