Ni Mara ngapi umekuwa ukiwapa watu muda wako? Ni mara ngapi umekuwa ukivipa vitu vya namna mbalimbali kwenye Maisha yako?

 

Umekuwa ukitumia muda mwingi na Tv au marafiki lakini ukasahau kutumia muda na wewe mwenyewe.
Umekuwa unatumia muda mwingi kazini kwako na kwenye shughuli zako nyingine lakini hupati nafasi ya kukaa na wewe pekee yako.
Katika Maisha ya sasa ili uweze kufurahia pia Maisha ni muhimu uwe unajipa nafasi ya kujisikiliza binafsi. Utambue nafsi yako inataka nini. Utambue mambo mengi makubwa uliyonayo. Kitu kimoja ambacho kinaweza kukufanya ujikute unapoteza mwelekeo wa Maisha ni pamoja na kukosa muda na wewe peke yako.
Kwenye Maisha ya sasa kuna Mambo mengi sana yanayotuvuta na kutuondoa katika utulivu wetu binafsi. Kuna mitandao ya kijamii na habari nyingi sana ambazo ukijikuta unazifuatilia utakosa muda kabisa wa kuwa na wewe mwenyewe.
Mafanikio ya kweli na yanayoleta maana yanaanzia ndani yako hivyo kama utakosa muda wa kukaa na kujitafakari mwenyewe ni ngumu sana kufikia mafanikio kwenye Maisha.
Hakikisha kila siku unapata nafasi ya kutafakari Maisha yako yanavyokwenda na vile vitu unavyovifanya. Kwa njia hii utajikuta unapata mawazo mengi sana bora kwa ajili ya kuboresha kile unachokifanya.
Njia mojawapo ya kuweza kujua kusudi la wewe kuwepo duniani ni kwa kupata muda wa kujisikiliza.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading