Haijalishi watu watasema nini juu ya Maisha yako, haijalishi wataongea nini kinachojalisha ni mwitikio wako kwenye yale maneno yao.

Haijalishi mtu amekutukana matusi makubwa kiasi gani kinachojalisha ni wewe umepokea kwa mtazamo upi. Vile unavyojiona wewe ina nguvu kubwa sana kuliko hata watu wanavyokutazama.

Haijalishi watakusifia kiasi gani au kukukosoa kiasi gani kama wewe mwenyewe hujiamini huwezi kufanya chochote.

Kabla hata hujalalamikia wengine kwenye matokeo unayopata jitazame mwenyewe kama kweli unaamini unachokifanya?  

Je unaamini ile ndoto yako kwa kiasi gani? Haijalishi unaemweleza atakupinga wewe nguvu ya Imani yako ni kubwa kiasi gani juu ya ndoto yako? mtu mmoja akasema kama vile ulivyo na uhakika juu ya jinsia yako ndivyo unavyotakiwa uwe na uhakika na Imani juu ya ndoto yako.  

Usikubali kuyumbishwa na watu wa nje. Ukiona maoni ya watu wa nje yanakurudisha nyuma ujue huna Imani ya kutosha juu ya ndoto yako. usikubali kuwa aina ya mtu ambaye hawezi kufanya jambo mwenyewe hadi watu Fulani wakubaliane nae.  

Jua kwamba kuna nyakati zinafika unataka kufanya maamuzi ambayo kila mtu atayapinga isipokuwa wewe mwenyewe. Mfano wazazi wako wamekusomesha kutoka shule ya msingi leo unamaliza chou wanatarajia unaenda kupata kazi nzuri wanashangaa unawaambia unakwenda kufanya kitu kingine tofauti kabisa na ulichosomea.

Tena unajiajiri na kutengeneza mwenyewe biahsara yako.   Wao wataona kama wamepoteza pesa nyingi sana kukusomesha leo hii wewe unafanya mambo ya ajabu.

Lakini kwasababu wewe unaamini ndoto yako unaweza kufanya makubwa. Lakini ukiwa mtu wa kusubiria maoni ya wengine ndipo uchukue hatua utakwama.   V

ILE UNAYOJIONA WEWE NDIO INA NGUVU ZAIDI KULIKO MTU MWINGINE YEYOTE ANAVYOKUONA.  

Jipatie Vitabu vya Biashara, Ujasiriamali na Mafanikio Hapa.

Jipatie Blog na Utengeneze Kipato kwa Njia ya mtandao hapa.  

#USIISHIE NJIANI  

Usiache kusoma Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO wasiliana nami kwa 0654726668.  

Jacob Mushi

Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.  

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading