Imekuwa ni tabia ya wengi kukutana na watu mnazungumza mengi sana kuhusu Maisha na wakati mwingine kufahamiana kwenye mambo mbalimbali ya Maisha. Sasa ni vyema uwe unajiuliza ukiwa peke yako je unapenda kumueleza nini mtu yule ambaye umekutana nae kwa mara ya kwanza?

Ungependa mtu huyu aondoke na picha gani kuhusu wewe? Hapa ni kutokana na kile mlichozungumza na sio jinsi alivyokutazama. Wewe unapendelea kusema nini au nini kisemwe juu yako kwa wengine?
Inawezekana umekutana na watu wengi sana kwenye Maisha yako na wengine walikuwa wawe sababu yaw ewe kusogea hatua moja kwenda nyingine lakini kwasababu ya kukosa kitu cha kujieleza ukajikuta umefeli.
Soma: Kitabu: Siri 7 za Kuwa Hai Leo ( Huu ni Mwongozo wa Kukuwezesha kutambua Kusudi la Kuwepo Hai)
Kama huna chochote unachokifanya kwa sasa ambacho ni utambulisho wako inakupasa uanze kuchukua hatua ili ufikie kwenye viwango vya kutambulika kwa kazi yako. Kusudi lako ndio utambulisho wako mkuu hapa duniani. Haijalishi umesoma mpaka wapi, umefanya kazi wapi, una vitu gani unamiliki ila kusudi lako ndio limebeba vyote.
Kwasababu kusudi lako lazima liwe linagusa Maisha yaw engine. Hivyo ni muhimu unapopata wasaa wakufahamiana na mtu kusudi lako wewe ndio liongoze hasa kwenye utambulisho wako. Watu wengi sana hawawezi kujitambulisha kwasababu hawajui kwanini wapo duniani.
Kamwe usikubali unapokutana na binadamu mwenzako ukamwacha akaondoka hivi hivi bila ya kumgusa kwa kile ambacho unakifanya hapa duniani. Unaweza kulitambua kusudi lako leo na ukaanza safari ya kulitimiza.
Hakuna Maisha mabaya kama Maisha yasiyo na makusudi, yaani kuishi bila ya kujua kwanini upo ndani ya dunia hii. Huwezi kutambua thamani yako kwa wengine ni ipi. Huwezi kutambua ni vitu gani ukivifanya unaweza kugusa Maisha yaw engine kwa ukubwa sana.
MTU YEYOTE UNAEKUTANA NAE UKAPATA NAFASI YA KUSHIRIKISHANA NAE, USIKUBALI AONDOKE BILA YA KUJUA KILE MUNGU AMEWEKA NDANI YAKO.


#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading