Ni rahisi kukua umri lakini sio kiufahamu.
Ni rahisi sana kukua kiumri kwasababu kila siku mpya unakuwa umeongezeka umri lakini kiufahamu unaweza kubaki palepale hadi uongeze kitu kipya kwenye ufahamu wako. Ni hatari sana kama utakaa kwenye mazingira yale yale, ukaendelea kufanya vitu vilevile, ukabakia unajua vitu vilevile. Utakua kiumri lakini kiufahamu utabakia pale pale. Jikumbushe mara ya mwisho kusoma kitabu ni lini?
Mara ya mwisho kutembelea sehemu mpya ni lini? Mara ya mwisho kufanya jambo la tofauti na uliyozoea kufanya ni lini? Ukiipata hiyo siku basi ujue hapo ndio mara ya mwisho kukua kiufahamu. Ndio maana unapata matokeo unayoyapata leo kwasababu hakuna kipya kilichoongezeka kichwani.
Ufahamu wa kitoto ni pale unapowaza kusaidiwa kila kitu kwenye Maisha yako. umepata tatizo hujafikiria chochote unawaza Fulani ndio anapaswa kukusaidia. Maendeleo yako ya nje yanaletwa na maendeleo yako ya ndani. Kama ndani umekwama hujakua utakutana na vikwazo vingi sana nje yako.
Unapokuwa hujui kitu Fulani ndio mtu anapata nafasi ya kukuongoza au kufanya chochote anachotaka kwako. Unapokuwa na ujinga kwenye ufahamu wako ndio unakuwa rahisi sana kudanganywa au mtu kuendesha maamuzi yako. hujawahi kuona watu wanaambiwa wafanye vitu vya ajabu na wao wanafuata tu hiyo yote ni kwasababu kuna mtu anaongoza fahamu zao.
Huwezi kuambiwa ule majani na unajua haya ni majani ukayala kama una ufahamu uliopo sawasawa. Matatizo mengi tuliyonayo yanaletwa na woga tulionao na taarifa tulizokosa kwenye ufahamu wetu. Ni rahisi sana mtu akayaongoza maamuzi yako kama una ujinga Fulani kwenye akili yako.
Kinachotutofautisha sisi na Wanyama wengine ni uwezo wetu wa kufikiri, kuuliza maswali, kuchunguza, kutaka kujua Zaidi. Usikubali kuwa mtu ambaye hajiulizi maswali hasa kwenye jambo ambalo limejificha jificha. Uliza maswali utapata majibu. Na popote penye uongo utapafahamu kwani watashindwa kukujibu.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading