HATUA YA 22: Unacho cha Kupoteza?

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Katika Maisha kuna mambo mengi sana huwa yanajitokeza na yanatufanya tuwe na hali za furaha au wakati mwingine hasira.

Juzi wakati nasafiri kwenda Mwanza, kwenye bus kulikuwa na mtu alilipa akaa kwenye siti mbele ya safari akaja kuambiwa ilikuwa na mtu tayari yupo kituo cha mbele hivyo asimame. Pale ndani ya gari kukatokea mabishano makubwa hadi askari wakaja kuingilia. Aliekalia siti hataki kutoka na mwenye siti anataka kukaa.

Mwishowe yule aliekalia siti ya watu ilimbidi akakubali kusimama. Nikapata nafasi ya kuongea nae wakati akiendelea kulalamika kuonewa akisema ataripoti mahakamani.

Kiukweli alikua ni mtu mzima kama baba yangu. Nikamuuliza kwani mzee wangu kuna kitu unapoteza usipokaa? Mwanza si tutafika? Nikamwambia hilo ni tatizo dogo sana lisikufanye uharibu Maisha yako na ya wengine.

Kitu cha kujifunza hapa ni kwamba wakati mwingine unaweza kuona umeonewa sana kwenye tatizo Fulani lililojitokeza, lakini kabla hujagombana sana na kulalamika jiulize kuna kitu nitakuwa na poteza?

Kama hakuna unachopoteza hakuna haja ya kuwa na hasira sana chukulia tu poa kama wasemavyo vijana. Acha tu lipite lisikuharibie siku.
Najua unaweza kufikiri utaonekana mjinga lakini ukweli ni kwamba kuna msemo unasema “hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu”
Kumbuka: kama kuna ambacho utapoteza usikubali kuacha kutafuta pia haki yako. Kama utakachopoteza kitaharibu maono yako usikubali kupoteza.

Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading