Kila mwanadamu amezaliwa akiwa amekamilika ndani yake. Hata kama atazaliwa bila ya viungo baadhi kwenye mwili wake lakini bado anakuwa amekamilika katika vitu vya muhimu sana kwenye maisha yake. Ni hatari sana kuwa na viungo vyote vya mwili halafu ukashindwa kutambua na kutumia mgodi ambao ulipewa wakati unakuja hapa duniani.

Mgodi huu unao na ni wewe pekee unaumiliki sio wote wameweza kutambua mgodi huu na vile vya thamani vilivyoko ndani yake.

Ni watu wachache wameweza kutumia sehemu ndogo ya utajiri ulipo ndani yao. Utajiri huu upo ndani ya ufahamu wako. Bila ya ufahamu au akili hakuna kitu chochote kilichogunduliwa na wanadamu kingeweza kutokea chenyewe. Hata madini ya dhahabu na almasi hayakutokea yenyewe yamegunduliwa na akili ya mwanadamu.

Kiungo pekee ambacho unakimiliki na ni cha thamani sana ni akili yako. Ukishindwa kutambua hivyo huwezi kujua ufanyeje. Unatembea na mgodi wenye thamani sana ndani yako. Bahati nzuri ni kwamba hakuna mwingine anaweza kuja kuchimba kwenye mgodi wako ni wewe mwenyewe uamue kufukua madini yaliyoko ndani yako au ubaki nayo.

Ukibaki nayo hasara ni ya kwako kwasababu huwezi kufikia mafanikio yeyote. Huwezi kufika popote unapotaka kama hujaamua kuanza kuchimba madini ya thamni yaliyowekwa ndani yako. Anza kuchukua hatua sasa utumie vitu vya thamani vilivyoko ndani yako ili upate Zaidi vile unavyovitaka.

Madini hayo ukiyatoa hutayafaidi mwenyewe lazima uwape wengine ndipo uweze kupata magari unayotaka, nyumba unazotaka, maisha unayotaka. Kama wewe una tabia ya uchoyo huwezi kufikia mafanikio kwasababu utakuwa unazuia vilivyoko ndani yako na hutapata ambavyo unavitaka.

Mgodi huu huwezi kuchimba dhahabu zake kama hutaki kujifunza. Ni sawa na umeambiwa kwenye mwamba huu kuna almasi kwa chini hivyo ni lazima uingie gharama ya kununua mashine ya kuvunja miamba ili ufikie almasi. Ndivyo ilivyo kilichopo ndani yako utaweza kukitoa vizuri kama utajifunza na kufanyia kazi yale unayojifunza kwenye maisha yako.

Ndugu yangu ukifa maskini ni makossa yako mwenyewe. Una kila kitu ndani yako. Unatembea na utajiri wako kichwani anza sasa kujifunza namna ya kufukua vile vya thamani ndani yako.

Kama utatumia muda mwingi kujaza uchafu ndani yako itakuchukua muda mwingi sana kufukua dhahabu iliyoko ndani yako. Acha kuingiza uchafu ndani yako kwasababu unapoteza vile vya thamani ambavyo vimejaa ndani yako. Badilisha unachoingiza ndani yako ndipo utaanza kuona thamani uliyoibeba. Soma vitabu, hudhuria semina, sikiliza audio na video za kukufundisha.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading