Ni ajabu sana kuona watu wakigombana kwasababu ya mali au vitu ambavyo vinaweza kupatikana kwa kutafuta kwa bidii.
Ni jambo la kushangaza kuona mtu anamchukia mwenzake kwasababu amemzidi kipato au kiwango cha mafanikio.
Inashangaza na kusikitisha mno kuona watu wanauana kwasababu ya vitu ambavyo vinaweza kupatikana endapo tu mtu atasimamia kile ambacho Mungu ameweka ndani yake.
Ukimchukia mwenzako kwasababu yeye ni maarufu kuliko wewe huo ni ujinga. Dunia ina watu wengi maarufu lakini nafasi za kuwa maarufu hazijajaa.
Ukisema unawachukia matajiri kwasababu wewe ni maskini utakuwa unapoteza muda bure kwani dunia bado inahitaji matajiri. Kwa vitu vya asili pekee vilivyoko huku duniani vinatosha kabisa kumfanya kila mmoja akatosheka na kile anachokitaka.
Dunia imejitosheleza imebeba utajiri ambao unamtosha kila mmoja. Yaani wewe kuwa maskini ni kwasababu tu hujajua namna ya kuzitumia fursa vizuri.
Hakuna sehemu ambayo haina fursa za kukufanya wewe uwe tajiri. Tukianzia ndani yako umejawa na vitu vingi ambavyo ukiweza kuvitumia utapata kila unachokitaka.
Acha kupoteza muda wako kujenga chuki zisizo na maana yeyote kwa waliokuzidi kipato, umaarufu na mali. Muda huo ungeuelekeza kwenye kufanyia kazi vile vitu Mungu aloweka ndani yako ungepiga hatua Zaidi ya hapo ulipo sasa hivi.
Ndugu yangu nikwambie ukweli dunia imejitosheleza kwa kila kitu hakuna binadamu anaepaswa kuishi maisha mabovu hapa duniani kwasababu dunia ina kila kitu.
Shida kubwa ipo pale unapotaka kupata bila ya kulipia gharama ya kile unachokitaka. Ukitaka utajiri lipa gharama halisi ya ule utajiri unaoutaka. Ukitaka umaarufu lipa gharama halisi ya ule umaarufu.
Soma: Simama pigana au Potea Kabisa
Hakuna maana yeyote kama tutaendelea kuuana kwasababu ya vitu ambavyo havina msingi wowote. Hakuna maana yeyote kama utajenga chuki kwa wenzako kwasababu tu wana kitu Fulani ambacho wewe huna. Unachopaswa ni kutumia ulichonacho vizuri.
Dunia imejitosheleza kwa kila kitu unachokitaka.
Ni mimi Rafiki Yako,
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/