Leo nataka ujiulize kwanini Mungu alikuumba wewe mwanadamu na wala sio kiumbe kingine chochote?

Ukijua hivyo huwezi kujidharau!
Ukijua hivyo huwezi kujifananisha na wengine!
Ukijua hivyo huwezi kukubali kushindwa!
Ukijua hivyo huwezi kukata tamaa kirahisi!
Utajua unapoelekea!
Utajua watu wakuambatana nao! 
Utajua ni vitu gani vya Kusoma!
Mnyama wa kawaida hua anawaza vitu viwili tu kula na kuzaliana. Lakini wewe binadamu umepewa uwezo wa kugundua vitu. Umepewa uwezo wa kufanya mambo makubwa!
Zaidi ya yote kila binadamu ana kitu cha pekee ndani yake. Yaani wewe ulizaliwa na kitu cha pekee sana ndani yako na kitu hicho chatakiwa kufanyika hapa duniani. Hakikisha huondoki bila kuacha athari duniani.
Kabla hujafa hakikisha kuna kitu umeacha duniani. Hakikisha dunia umeipendezesha kwa ugunduzi wako.
Yote haya yanawezekana kwa kutambua kwanini hukuzaliwa mnyama mwingine yeyote ukazaliwa binadamu.
Umeshatambua kwanini Wewe ni mwanadamu na sio kiumbe kingine?
Anza kuchukua hatua leo kufikia ndoto zako weka malengo ya vile vitu unavyotaka kuvifikia.
Fanyia kazi malengo yako.
Bila kukata tamaa.
Utafikia kule unapoona.
Sifa ya mwanadamu  ni uwezo wa kuona mbele yaani maono. Kwa kuangalia hali iliyopo sasa unaweza kutambua ni nini kitatokea miaka mitano ijayo.
Vitendo ni muhimu. Maarifa ni muhimu.
Utafikia kile unachokiona
”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger,
Simu: 0654 726 668,
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading