HATUA YA 240: Tatizo Lipo Ndani Yako.

Nimekutana na watu wenye uwezo mdogo, wana kiwango kidogo lakini wanafanya mambo makubwa sana.

Wapo ambao hawana elimu kubwa uliyonayo wewe lakini wamefika mbali sana.

Kuna wengine hawana wazazi wazuri kama wako lakini wamepiga hatua kubwa sana.

Kinachokufanya ubaki hapo ulipo ni wewe mwenyewe. Unajiona kwamba huwezi, unaogopa changamoto ambazo utapitia njiani.

 

Ni kweli unataka mafanikio lakini unaogopa kushindwa, unaogopa ukubwa wa kile unachokitaka. Haiwezekani ukapata mambo makubwa bila ya kupitia kwenye mchakato. Hakuna kitakachotokea kama muujiza.

 

Lazima ubadilishe mtazamo wako unaokuzuia kwenda hatua nyingine.

Lazima ukubali kupitia mchakato.

Wengi tunataka Baraka lakini hatutaki kulipa gharama za Baraka.

Tatizo ni wewe umekubaliana na hali uliyonayo na umeona unastahili kuwepo kwenye hatua uliyopo sasa hivi.

Ili upate matokeo tofauti na unayopata sasa hivi lazima ukubali kubadilisha ufahamu wako.

 

Watu wengi wanaogopa makubwa kwasababu ya gharama ya kutunza yale makubwa. Unajua unaweza kupata makubwa ndio lakini yasidumu kwako kwasababu hujaweza kutunza.

Gharama za kupata makubwa pia zinaweza kuwa kikwazo cha wengi kusogea mbele. Watu wengi wanaogopa kwenda hatua nyingine kwasababu ya gharama wanazopaswa kulipia.

 

Unachotakiwa kuelewa ni kwamba huwezi kujua kuogelea vizuri kama unaogopa misukosuko ya kwenye maji. Huwezi kupata mtoto kama unaogopa kubeba ujauzito, au unaogopa uchungu.

Lazima ukubali kubadili mtazamo wako ndani uondokane na hofu inayokuzuia kwenda mbele.

Usikubali wewe mwenyewe uwe kikwazo kwako.

Usikubali mawazo yako yawe sababu ya wewe kushindwa kusonga mbele.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. www.jacobmushi.com/jiandikishe

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. www.jacobmushi.com/vitabu

Jipatie Blog Bora hapa.. www.jacobmushi.com/jipatieblog

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading