Ni kweli tukio la siku moja linaweza kubadilisha sura ya maisha yako kabisa yalivyo kuwa kwenda kwenye historia nyingine. Tukio hili la siku moja linaweza kuwa sababu ya maisha yako kubadilika na watu wakasahau kama ulikuwa na maisha Fulani kabla.

Katika tukio hili linaweza kuwa hasi au chanya.

Tukio hasi linaweza kuwa ajali, au umefanya kitendo kiovu na ndani ya siku moja maisha yako yote yakabadilika kwenda kwenye sura nyingine.

Kwa kupitia ajali ya siku moja maisha yako yanaweza kubadilika sura kabisa ukaishia kitandani siku zote za maisha yako zilizobakia. Tukio la siku moja linaweza kuwa sabababu ya wewe kupoteza viungo vyako vyote.

Labda umefanya kitendo cha ubakaji maisha yako yote yanaweza kuhamia jela kwa tukio la siku moja tu. Umefanya kitendo cha zinaa maisha yako yote yakaharibika kwa kupata maradhi. Ogopa sana tukio la siku moja.

Kama kuna namna ambayo unaweza kuzuia tukio ambalo unajua linaweza kubadilisha sura ya maisha yako na kwenda kuwa mabaya kabisa ni bora ukafanya hiyo namna. Usikubali kuwa kwenye eneo ambalo litakupelekea kupata vishawishi vya kufanya tendo baya litakaloharibu maisha yako.

Mara nyingi watu huita hii ni bahati mbaya au mikosi.

 

Tukija kwenye tukio la siku moja chanya inawezekana kabisa likatokea na kubadilisha maisha yako. Lakini sasa inakubidi uwe una kitu unafanya ili kiweze kukuunganisha na tukio hilo.

Ili tukio chanya la siku moja litokee kwenye maisha yako lazima uwe una kitu unakifanya. Hivi unajua huwezi kuokota pesa ndani kwako? Ili uipate bahati ya kuokota pesa unatakiwa uwe umetoka ndani ya nyumba yako uwe barabarani.

Ninaweza kusema ili mpiganaji wa ngumi aweze kushinda na maisha yake yabadilike ndani ya pambano moja tu lazima awe ameshafanya mazoezi ya kutosha. Lazima awe ameshapigana mechi ndogo ndogo za kutosha. Hivyo ili na wewe liweze kutokea hilo tukio lazima kuwe kuna kitu unafanya.

Ili uweze kupata mtu atakaebadili historia ya biashara yako hupaswi kukaa sehemu moja na kumsubiria, unapaswa kuwa kwenye mchakato na njia zitafunguka za kumfikia mtu huyo.

Matunda ya kazi unayofanya kila siku ipo siku yataonekana. Ipo siku utasahau yote unayopitia sasa hivi. Ipo siku utaanza kutoa hadithi ya haya unayopitia sasa hivi.

Ili tukio la siku moja litokee kwenye maisha yako lazima kuwepo kitu unachokifanya na kinachokutambulisha wewe. Ipo siku usiyoijua bidi zako zitaonekana na zitaleta mabadiliko kwenye maisha yako.

Kama hauna kitu kinachokuweka bize usikae usubiri hilo tukio la siku moja lije libadilishe maisha yako. Ni sawa na kusubiri uokote pesa wakati upo ndani kwako. Huwezi kufananisha anaesubiri embe chini ya mnazi unajua hata nazi ikianguka hatakuwa sawa na wewe uliye ndani atapata nazi.

Tafuta kitu cha Kufanya Bahati hazitokei zenyewe zinatengenezwa. Kama unataka atokee mtu mkubwa kwenye maisha yako halafu maisha yako yabadilike basi tafuta kitu cha kufanya na ukifanye kwa bidii hadi watu wakushangae

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. www.jacobmushi.com/jiandikishe

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. www.jacobmushi.com/vitabu

Jipatie Blog Bora hapa.. www.jacobmushi.com/jipatieblog

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading