Moja ya makosa ambayo unaweza kuyafanya kwenye maisha yako ni kutokujua ni wapi unakwenda. Kitu cha pili ambacho utakuwa unaendelea kukosea ni unapojua unataka kuwa nani halafu basi ikaishia hapo hakuna chochote unachokifanya kinachoelezea kile unachotaka kuja kuwa.

Kitu cha tatu ni kutokuwa na malengo na mipango iliyoandikwa na unaifanyia kazi kila siku. wengi ukiwauliza unataka kuja kuwa nani? Watakujibu vizuri sana, Ukiwauliza kuna mahali umeandika hicho kitu? Utakuta ni wachache sana katika kumi anaweza kuwa mmoja alieandika.

Tatizo jingine usiishie kuandika ukaweka kitabu chini ukaondoka. Unapaswa kujua ni nini kifanyike ili utoke hapo ulipo ufike kule unakotaka kuwa. Unajua ili ufaulu mitihani hutakiwi kuandika notes zote na ukajaza madaftari bali ni kwa kusoma kile ulichokiandika na kufanya mazoezi ya maswali mbalimbali.

Kitu kingine umeshaandika na unafanyia kazi hayo unayotaka yatokee kwenye maisha yako, unakosea sana ukifanya mwenyewe. Tafuta mtu wa kukuongoza na kukufundisha. Tafuta marafiki ambao wanafanana na wewe, wanataka kufika kule unakotaka kufika.

Kitu kingine unapaswa kufanya kila siku hicho ulichoamua kufanya hadi ufikie kule unakotaka kufika. Hakuna mpiganaji anaepatia ushindi kwenye ulingo, ushindi unaanzia kwenye mazoezi akiwa peke yake. Uwanjani unakwenda kukamilisha ulichokuwa unafanya nyuma ya pazia.

Ufaulu hautokei siku ya mtihani bali unakuwa kwenye maandalizi. Sasa muda huu ambao hakuna mtu anakufahamu ndio unapaswa kuweka nguvu kubwa , na juhudi za kutosha ili uweze kufanya mambo makubwa kwenye mwisho wako.

Wengi wetu tunataka ushindi wa jukwaani, hakuna kitu kama hicho lazima uweke juhudi huku nyuma ya pazia ambapo hakuna anaekuona. Huku chini watu hawatakusifia lakini ukifika jukwaani ukapata ushindi kila mtu atakushangilia.

Vikwazo vyote unavyokutana navyo visikufanye ushindwe kukua. Visiwe sababu ya wewe kuaihirisha ndoto zako. Mvua zikinyesha kama mtoto alitakiwa kutembea ataendelea kujifunza tu hata kama kuna utelezi.

Kitu cha mwisho unapaswa kutambua kwamba hakuna mafanikio yanayopatikana kirahisi hata siku moja. Hilo lifute kwenye akili yako, sehemu yeyote duniani mambo makubwa yanapatikana kwa kuweka nguvu kubwa bila ya kuchoka wala kukata tamaa. Hivyo unapoona ugumu tambua ndio asili ya mafanikio hiyo. Udongo haiwezi kukaa kwenye mlima milimani inakaa miamba. Udongo mlaini huwa unapelekwa tambarare.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading