Kama kuna kitu umeamua kukifanya unachotakiwa ni kuchukua hatua sasa na kuanza. Mara nyingi wengi wanasema nitaanza tu, lakini baada ya muda ukimuuliza vipi ile biashara umeanza? Umeshaanza kufanya kile kitu? Watakwambia hapana.

 

Unapotumia muda mwingi kukichunguza kitu utaanza kupata hofu na hofu itakuzuia wewe kuanza kuchukua hatua.

Unapochunguza sana utaanza kuona kutokuwezekana na utaingia na woga na mwisho wake utaishia kuahirisha tu.

Hauwezi kujua kila kitu kama hujaanza kufanya. Huwezi kujua kila kitu kwa kufuatilia na kuuliza. Mambo mengine yanatokea katikati ya safari.

Kuna msemo unasema ukimchunguza sana bata hutamla. Hii ni kwasababu utakutana na tabia ambazo hujawahi kuzijua. Utakutana na mambo ambayo hukuwahi kuyatarajia na mwisho wako yatakukatisha tamaa.

 

Unataka kufanya jambo hakikisha una taarifa za muhimu tum engine achana nayo utakutana nayo mbele. Kutaka kujua kila kitu ndio sababu ya wengi kuahirisha ndoto zao.

Huwezi kutoka hapo ulipo kama hujaamua kupiga hatua ya kwanza ambayo ni uthubutu.

Huwezi kupata chochote kile kama hujaamua kuchukua hatua.

Amua kuanza sasa kuiishi ile ndoto yako.

Kadiri unavyoahirisha ujue unayaairisha maisha yako.

Huo muda unaopoteza hautakaa urudi tena.

Anza sasa, Chukua Hatua.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. www.jacobmushi.com/jiandikishe

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. www.jacobmushi.com/patavitabu

Jipatie Blog Bora hapa.. www.jacobmushi.com/jipatieblog

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading