HATUA YA 245: MVUA NA JUA.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Kama ilivyo vipindi na majira ya mwaka kuna nyakati kuna mvua na kuna nyakati kuna jua vilevile ndivyo yalivyo maisha yetu. Haiwezekani ukasema unataka jua liwake tu siku zote kwasababu mvua sio nzuri pia huwezi kusema mvua zinyeshe siku zote kwasababu hulipendi jua.

Mvu zinaponyesha zina maana yake zinarutubisha mazao na mimea mbalimbali hata kama hulimi lazima utakuwa unakula chakula kilicholimwa na kunyeshewa na mvua. Hivyo mvua si kwa ajili ya wakulima pekee inaponyesha ni yetu sote.

Jua linapowaka linahusika katika shughuli mbalimbali hata kama unalichukia vipi jua huwezi kulizuia lisiwake kwasababu kuna viumbe vingine vinafaidika na kuwaka kwa jua.

Katika maisha yako hupaswi kuchukia au kukasirika kwa hali yeyote mbaya inapotokea. Hakuna hali inayotokea yenyewe kwenye maisha. Ukisema wewe unataka kuishi bila ya kupitia matatizo ni sawa na kusema usiishi hapa duniani.

Mvua zinaponyesha ili kurutubisha mimea kuna watu wanaathirika na mvua hizo lakini suluhisho sio kuziondoa mvua bali ni kuweza kukaa sehemu ambayo mvua haitakuletea madhara makubwa. Ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu changamoto tunazopitia haiwezekana zikaisha ukaishi bila misukosuko yeyote.

Kila Hatua ya maisha ina changamoto zake. Ukifikiri ukifikia viwango Fulani vya maisha hautakuwa na changamoto basi utakuwa unajidanganya. Unachotakiwa kuelewa ni kwamba changamoto unazopitia sasa hivi ni za kiwango ulichopo. Kadiri unavyozidi kupanda unabeba makubwa Zaidi ya uliyopo.

Kama wewe unaogopa matatizo huwezi kamwe kukua na kufikia viwango vya juu. Yeyote alie juu anatatua matatizo makubwa Zaidi. Kama unataka kwenda juu kuwa tayari kubeba na kutatua matatizo makubwa Zaidi.

Maisha bila ya changamoto ni sawa na dunia bila ya mvua au bila ya jua kikikosekana kimoja ukuaji wa viumbe unakwama ndio maana jangwani huwezi kukua kijani kibichi kwasababu kuna jua Zaidi. Vilevile baharini huwezi kuona miti inaota kwasababu kuna maji peke yake.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. www.jacobmushi.com/jiandikishe

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. www.jacobmushi.com/patavitabu

Jipatie Blog Bora hapa.. www.jacobmushi.com/jipatieblog

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading