Ukitaka watu wakuchukie waambie ukweli.

Ukitaka kupingwa na kila mtu simamia ukweli.

Ukitaka kupata wafuasi wachache wewe simamia ukweli wale wanaopenda kudanganywa wataona huwafai.

Mara nyingi jambo ambalo linapata wafuasi wengi sana kwa haraka huwa najaribu kuangalia kwa macho ya ziada kama ni la kweli kwasababu wengi wengi hatupendi ukweli.

Mara zote tunapenda mambo marahisi ambayo kiukweli hayana faida yeyote kwenye maisha yetu Zaidi ya kutupa faraja ya uongo.

Ukitaka watu waache wanavyofanya na wastaajabu kwa kile ulichokifanya wewe simamia kile unachokiamini bila kuyumbishwa.

Ni watu wachache sana wanaoweza kusimamia ukweli. Ukweli ndio sababu ya maumivu mengi ndani ya maisha ya watu.

Baada ya kuujua ukweli kwamba ulikuwa unadanganywa kwamba unapendwa ndipo mtu huanza kuumia na kupata vidonda vya moyo.

Kwanini watu wanauogopa Ukweli?

Ukweli unakuwa ni sawa na kumuweka mtu wazi mbele za watu.

Ukweli unamfanya mtu anakuwa uchi kwa yale matendo yake maovu.

Ukweli unafunua vilivyofunikwa.

Ukweli ndio njia pekee ya kuonyesha maovu ya watu.

Sasa kwasababu tuna watu wengi waongo na wanaoishi maisha ya kuigiza na unafiki wa hali ya juu unaposimamia ukweli utakutana na maadui wengi.

Maadui hawa wanakuchukia kwasababu unataka kwenda kuwavua nguo zao za uongo walizovaa kufunika uhalisia wao.

Ukweli Kuhusu Ukweli.

Ukweli utakuweka huru. Mithali moja inasema unapokuwa mkweli huna haja ya kukumbuka vitu kwasababu ni ukweli. Huna haja ya kuwa na mambo ya gizani.

Ukweli utakufanya uishi maisha ya furaha hapa duniani. Unapokuwa mkweli huwezi kuishi maisha ya wasiwasi kwasababu ya mambo unayofanyia gizani unahisi watu watakuja kuyajua siku moja.

Unapokuwa mkweli unaondokana na hofu. Hofu juu ya mambo ambayo umekuwa unayaficha. Hofu ya maovu uliyotendea watu.

Usiogope kabisa unapoufahamu ukweli. Kama kuna mtu alikuwa anakudanganya ukaja kufahamu ukweli usiumie furahia uhuru wako. Furahia kuondoka kifungoni. Ni bora umetambua hivyo kuliko kuendelea kudanganywa.

Ukweli hauhitaji maneno mengi. Mara nyingi ninapoona mtu anatumia nguvu nyingi kulazimisha aeleweke au mtu amuelewe hua Napata wasiwasi labda anadanganya maana ukweli hauhitaji mtu wa kuutetea mara nyingi unasimama wenyewe.

Ukweli Unauma ndio maana watu wapo tayari kuua ili tu wabakie na yale waliyoficha ndani yao.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading