HATUA YA 249: Kwanini Unahitaji Watu wote? (Wanaokupenda na Wasiokupenda)

#SITAISHIA_NJIANI

✈-Napiga hatua kuelekea mafanikio yangu.

❗-Navumilia kila hali na changamoto nitakayopitia njiani.

?-Najifunza kila siku na kuweka kwenye matendo yale ninayojifunza.

??-Naweka juhudi na bidii kwenye kila ninachokifanya kwa mikono yangu.

Mafanikio ni Haki Yangu.

Eeh Mungu niwezeshe.

?Mimi ………

Unawahitaji watu wote kwenye maisha yako kwasababu kila mtu ana jambo akilifanya kwako lin akusababisha wewe usonge mbele.

Watu wabaya wanakuwa sababu yaw ewe kusonga mbele Zaidi na kujifunza jinsi ya kuishi vizuri na watu. Mfano mtu akitokea akakutapeli utajifunza kuwa makini Zaidi na kutowaamini watu hovyo.

Nyuki na wadudu wengine ni mara chache kuwaona mti unapotoa matunda yake. Mara nyingi wadudu hawa wabaya kwa wazuri hutokea kwa wingi sana miti inapotoa maua.

Kama mti utasema hawa wadudu ni wasumbufu kwangu siwataki basi kamwe tusingelikula matunda. Maua yangepukutika chini. Hivyo wakati mwingine kila mtu ana sababu ya kuwepo au kutokea katikati ya safari ya mafanikio yako.

Unatakiwa uelewe kwamba watu wengine wanakuja kukufanya uongeze mwendo. Watu wengine Mungu anawaleta kukuonyesha kwamba hapo ulipo sio mahali pako hivyo wanakusumbua ili uhame hapo uende viwango vingine vya juu Zaidi.

Ukiendelea kuwa na watu wanaokupenda tu na kukusifia huenda hutasonga mbele utabaki hapo ulipo kwa muda mrefu Zaidi. Mwiba unapokuchoma unakukumbusha kuvaa viatu na sio kukuzuia kuendelea na safari.

Nataka utambue kwamba watu wote wanahitajika kwenye maisha yako na wakati mwingine ni kupima ukomavu wako. Wanakuja watu kukusema vibaya, wengine watasema hujui unachokifanya, wengine watasema unaringa, wengine watasema wewe mchawi, wengine watasema ulihonga ndio ukapata hicho cheo ulichonacho.

Lakini yote hayo ni kupima je wewe umekomaa? Unaweza kuyabeba hayo yote? Unaweza kuvumilia? Kama kweli wewe unachokifanya ni chako huwezi kuchoka na kukata tamaa. Mti haujawahi kuwafukuza nyuki kwasababu ni wabaya. Na ukiona mtu umewafukuza nyuki ujue mwisho wa kutoa matunda umekaribia.

UNAWAHITAJI WATU WOTE KWENYE MAISHA YAKO. WENGINE NI KWA AJILI YA KUKUSUKUMA UTOKE HAPO ULIPO. WENGINE WATAKUCHAPA NA VIBOKO ILI UKIMBIE.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading