Kama ulikua hujui kwenye hii dunia kila binadamu anauza. Kila mtu kuna kitu anauza au kama hauzi basi hajajua kama anauza.


Unatakiwa ujue ni kitu gani hasa unakiuza ili uweze kukiuza vizuri.
Unatakiwa ujue unaemuuzia ni mtu wa namna gani!
Hata kama una bidhaa nzuri kiasi gani kama humjui mteja wako huwezi kuuza vizuri au kabisa.

Mteja wako ndiye anaefanya biashara yako iwe na uhai.
Kama hujui hilo unatakiwa utambue kuanzia sasa.

Ukitumia muda mwingi katika kutengeneza bidhaa yako nzuri ukasahau kumfanya mteja aendelee kuwa wako biashara yako itapoteza nguvu.

Jitahidi sana kutambua unauza nini na ni nani unamuuzia ili uweze kuuza vyema. Kama kuna chochote unafanya na unaingiza pesa hapo ndipo unapouza inawezekana unauza ujuzi wako kwa mwajiri au mtu mwingine.
Jifunze namna ya kuuza vizuri ndipo kwenye mafanikio makubwa.

Wengine wanauza vipaji, maarifa, nguvu, muda, na kadhalika. Hakikisha umejua unauza nini. Hakikisha umemjua mteja wako na jifunze namna ya kumfanya abaki kwako moja kwa moja.
Mteja wako ndiye anakuweka mjini sio bidhaa yako. Kama una bidhaa nzuri na huna wateja haina maana.

KUMBUKA: NI MUHIMU SANA KUWA NA BIDHAA BORA KABISA LAKINI UNATAKIWA UTAMBUE NI NANI HASA UNAEKWENDA KUMUUZIA. MTEJA NDIO ANAKUWEKA MJINI. MLINDE MTEJA WAKO KULIKO BIDHAA YAKO.

Karibu sana.

”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading