Tofali hujengwa kwa mkusanyiko wa punje moja moja za mchanga ambazo unaweza kuzibeba mkononi mwako lakini hujenga tofali ambalo huwezi kulibeba kwa mkono mmoja. Tofali nalo hujenga ghorofa kubwa sana ambalo binadamu na mali nyingi za thamani hukaa humo.

Hadi unaliona jengo kubwa la ghorofa linalotokea lilianza kwa mkusanyiko wa punje ndogo sana ya mchanga. Inawezekana ukaidharau punje ndogo ya mchanga lakini bila hiyo ghorofa zuri unalolisifia usingeweza kuliona limesimama.

Imekuwa ni kawaida sana kwa watu kudharau vitu vidogo vidogo ambavyo wanatakiwa kuvifanya kwenye maisha yao ili wajenge mafanikio na maisha bora. Imekuwa ni kawaida ya wengi kuona kwamba kazi Fulani haiwezi kunifaa kwasababu mimi hadhi yangu ni hii au ile.

Kumbe vile vitu ambavyo unaviona havina maana au ni vitu vya chini sana ndio vimewafanya watu wakubwa wakafikia sehemu zile walizopo sasa hivi.

Unaweza kuidharau shilingi mia moja ambayo mtu anaipata kwenye karanga lakini kuna tajiri mmoja anauza biskuti ya shilingi mia kwa mamia elfu ya watanzania kila siku.

Unapata Madhara Gani Ukidharau Vitu Vidogo Vidogo?

Kwanza unabakia kwenye hali uliyonayo siku zote kwasababu huwezi kutoka hapo ulipo bila ya kuanza kwa hatua moja.

Maendeleo yako yanarudi nyuma kwasababu kama dunia inasonga mbele na wewe umesimama unasubiri muujiza Fulani utokee ni kwamba hata waliokuwa nyuma yako watakuja na kukupita.

Madhara makubwa yatakukuta hapo ulipo kwasababu unaogopa kuthubutu, chukua hatua sasa weka aibu zako pembeni anza na ulichonacho.

Madhara ya Tabia Mbovu Ndogo Ndogo.

Tabia mbovu ndogo ndogo huleta madhara makubwa sana kwenye maisha yetu. Teja hawi teja ndani ya siku moja bali ni kadiri anavyojaribu kila siku kuonja unga.

Kadiri unavyozembea kufanya mazoezi unajietengenezea afya mbovu.

Kadiri unavyoendelea kupenda vitu vya anasa unajitengenezea umaskini mbaya sana hapo baadae.

Mwili wako umejengwa na mifumo midogo midogo ambayo inasababisha mwili wako unaweza kufanya kazi.

Naomba utambue kwamba maisha yako yanajengwa na mkusanyiko wa vitu vidogo vidogo unavyofanya kila siku.

Ukitaka kutengeneza mfumo mkubwa wa biashara ambao unakutengenezea pesa anza kidogo kidogo. Usikimbilie mwisho kabla hujaanza mwanzo.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading