HATUA YA 253: Hizi Ndio Nyakati za Kujua Kwanini Ulianza Unachokifanya.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Kwenye maisha kuna nyakati huwa zinatufikia ambazo zinakuwa ni kipimo ambacho kinaonyesha ukweli wa makusudi yetu kwa yale tuliyokuwa tunataka au tayari tunafanya. Unaweza kukutana na changamoto kubwa kiasi kwamba ukafikia hatua za kusema kama hali ni hii basi sifanyi tena hiki kitu.

Lakini ukweli unabaki pale pale kwanini uliamua kufanya? Kabla hujakata tamaa ni vyema ukaanza tena kujiuliza ni kitu gani hasa kilikusuma wewe kuamua kuanza hiyo biashara? Hicho kipaji chako? Hilo kusudi lako?

Ukiweza kukumbuka vyema sababu ambazo zilikuwa zinakusukuma wewe kuchukua maamuzi ya kuanza unaweza kuendelea mbele au kuamua kuacha.

Kuna nyakati zinakuja hata wale uliowategemea labda wangesema chochote japo kukutia moyo kwa wakati mgumu unaopitia na wao wakakaa kimya kabisa.

Kuna nyakati ulitegemea watu Fulani labda wangekupa msaada kwa juhudi ulizoonyesha ukaja kugundua kumbe na wao walikuwa wanakupiga vita sana.

Kuna nyakati utakuja kugundua hata wale watu wako wa karibu sana hawaamini hata kidogo kwenye ndoto zako tena wanakusema kwa pembeni huyu jamaa na ndoto zake.

Hizo ndio nyakati hasa za kupima wewe unawezaje kusimama? Unaweza kweli kusimamia kile unachokiamini?

Unaweza kweli kuipigania ndoto yako bila ya kuogopa watu wanasemaje, wakubali au wakatae?

Huu ndio wakati wa kuwaonyesha kwamba inawezekana hata kama walisema haiwezekani.

Huu sio wakati wa kukata tamaa huu ndio wakati wa ushindi ukiweza kuvuka changamoto hii lazima utoke. Lazima uwe na hadithi nyingine.

Endelea kusimamia unachokiamini haijalishi ni nani anakikubali au ni nani anakikataa.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading