HATUA YA 252: Uko Hivyo Ulivyo Kwa Kuamua.

jacobmushi
2 Min Read

Wako waliopitia changamoto kubwa kuliko wewe lakini hawajakata tamaa. Wako ambao walipata hasara kubwa sana kuliko hyo ambayo unajitetea nayo lakini bado wakasonga mbele na sasa tunazungumzia mafanikio yao makubwa.

Wako waliochwa na waale waliowapenda sana lakini hiyo haikuwa sababu ya wao kuacha kutimiza ndoto zao bado wakasonga mbele tu. Hiyo kwao haikuwa sababu kubwa sana kwasababu waliamua na wako tayari kupambana na changamoto yeyote ambayo itakuja mbele yao.

Rafiki yangu nikwambie kwamba uko hivyo ulivyo kwa kuamua. Hali yeyote inayoendelea maishani mwako umeikubali wewe iwe kikwazo kwako ungeweza kuamua isiwe kikwazo.

Uko hivyo ulivyo kwasababu ulikubali kuzipa changamoto nafasi ya kuonekana kubwa kuliko ndoto zako. Unajua wapo ambao walianza na wakafika hatua kubwa sana halafu wakapoteza kila kitu lakini wakainuka tena kuanza upya na bado wakafika mbali Zaidi ya walipokuwa mwanzo.

 

When something is important enough, you do it even if the odds are not in your favor. Elon Musk


Umuhimu wa ndoto zako na maono yako unatakiwa uwe mkubwa kuliko sababu yeyote ambayo inaweza kujitokeza mbele yako.

Ukiona umepata sababu za kujitetea na kuacha kuendelea kupigania ndoto yako ujue tu hiyo ndoto haikuwa ya muhimu sana. Kama ingekuwa ni ya muhimu usingekubali chochote kikuzuie labda kifo pekee yake.

Unaweza ukaja kwangu ukajitetea na sababu mia kwanini umeshindwa kwanini haiwezekani, kwanini ulikata tamaa, lakini mwisho wa siku nitakuuliza maono yako, ndoto zako ni za muhimu kiasi gani kwenye maisha yako?

Kama unaweza kuziona sababu ndio zina umuhimu Zaidi kuliko hata ndoto zako basi inaonekana hukuamua kuwa tayari kupambana.

Ukiweka sababu mbele sababu zitakuja nyingi sana. Ukiweka ndoto yako mbele yako uwezekano wa kuendelea utauona.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading